MCHEZO wa
ligi ya taifa daraja la nne manispaa ya Morogoro kati ya timu ya
Terminal inayomilikiwa na wapiga debe wa stendi ya mabasi ya Msamvu na
timu ya Compassion inayomilikiwa na kanisa la Aglikana umevunjika
dakaika ya 20 baada ya mvua kubwa kunyesha muda mfupia baada ya mchezo
huo kuanza.Hali hiyo ilisababsiha uwanja wa saba saba kujaa maji na
kusababsiha wachezaji kushindwa kumuiliki mpira huku wachezaji hao
wakianguka hovyo.Mvua hiyo ambayo mapaka sasa inaendela kunyesha
ilisababisha uwanja huo kujaa maji hivyo mwamuzi wa mchezo huo
aliyefahjamika kwa jina moja la Simba baada ya kujadiliana na uongozi wa
kamati ya ligi hiyo alimu kuvunja mchezo huo dakika ya 20.Kaimu
mwenyekiti wa chama cha soka manispaa ya Morogoro Boniface Kiwale
alipotakiwa kuelezea hatima ya mchezo huo alidai kwamba utaludiwa siku
nyingine.
mchezo huo ukiendelea kwenye madimbwi ya maji
Hadi
mchezo huo unavunjika timu hizo zilikuwa hazijafungana huku Terminal
wanaongoza ligi hiyo walioneka kumilika mpira kwa dakika zote 20.Ligi
hiyo itaendela kesho kwa Mawenzi market inayomilikiwa na wafanyabiashra
wa soko la matunda la Mawezi ambao wanashika nafasi ya pili kwenye
msimamo wa ligi hiyo watakipiga na Sultan Area inayosbuluza mkia kwenye
ligi hiyo
Baada
ya mvua hiyo inayoendelea kunyesha kwa sasa mwamuzi wa mchezo huo
aliyefahamika kwa jina moja la Simba akitoka uwanjana na kwenda
kujadiliana na makati ya ligi hiyo kufuatia uwanja huo wa saba saba
kujaa maji
Wachezaji wakisubili wakati wajadiliano hayo yakiendelea
Baada
ya kujadiliana na uongozi wa kamati ya ligi hiyo mwamuzi Simba,aliamu
kuvunja pambano hilo baada ya uwanja kujaa maji,picha mwamuzi huyo
akichukua mpira kwa lengo la kuvunja mchezo huo.
No comments:
Post a Comment