Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.Majid Mjengwa.
DAR ES SALAAM:
MWANDISHI
wa safu katika magazeti mbalimbali nchini, Majid Mjengwa amekamatwa na
polisi kwa tuhuma za kuhusika na tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda.
Habari
zilizolifikia gazeti hili jana mchana na baadaye kuthibitishwa na polisi
zinasema Mjengwa alikamatwa muda wa asubuhi na kwamba alikuwa akihojiwa
na makachero wa jeshi hilo hadi alasiri kuhusu tukio la kuteswa kwa
Kibanda.
Msemaji Mkuu wa Polisi Advera Senso aliliambia Mwananchi kwamba:
“Ni kweli
kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji, tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi
ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”
Hata
hivyo, Senso hakuwa tayari kueleza kwa undani muda aliokamatwa Mjengwa
wala sababu za kukamatwa na kuhojiwa kwake, lakini chanzo chetu ndani ya
Jeshi la Polisi kilithibitisha kwamba pamoja na mambo mengine kuhojiwa
kwake kulihusu uteswaji wa Kibanda.
SOURCE AUDIFACE BLOG
SOURCE AUDIFACE BLOG
No comments:
Post a Comment