|
H. Baba akionesha pipi zake. |
Katika
kuonesha kwamba bado ana kiu ya kuona sanaa yake inapanuka na kuvuma
mbali huku akiboresha maisha yake, kukuza kipato na kuongeza ufanisi , msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini H. Baba ameamua kujikita
katika biashara kwa style ya kipekee kwa kuingiza sokoni bidhaa aina
ya pipi zenye jina, picha na chata zake, pipi zinazojulikana kwa jina
la "H. BABA & FLORA MAPENZI KWA WATOTO".
Pipi
hizo zilizopambwa kwa picha ya H. Baba katika karatasi ya kuishika
pipi, zikipambwa na mfuko wa nylon wenye uzito wa gram 250 uliona picha
ya mwanamuziki H. Baba na mwigizaji wa Bongo movie Flora Mvungi na zinazo
tengenezwa na kampuni ya TANFRIK LIMITED ya Nairobi nchini Kenya, tayari zimeanza kuuzwa kwenye baadhi ya maduka na vibanda mbalimbali vya biashara kanda ya ziwa.
|
Muonekano wa mbele. |
|
Muonekano wa nyuma. |
No comments:
Post a Comment