Wakati Rais mpya wa Kenya Uhuru Kenyatta BAAD ya kuapishwa kuiongoza nchi hiyo, nimeipata ripoti ya kituo cha TV cha NTV inayoonyesha jumba lililojengwa na Serikali ya Kenya kwa ajili ya kumzawadia Rais Kibaki anaestaafu.
Ripoti ya NTV imeasema kwamba kuna uwezekano Rais huyo akaja kuishi kwenye nyumba hii iliyopo Mweiga Nyeri nchini humo japo pia kuna taarifa nyingine zinasema kwamba Rais huyo hapendelei maisha ya kijijini, zaidi anapenda mjini.
Mwai Kibaki mwenye umri wa miaka 81, anamiliki nyumba tatu za kifahari kwenye jiji la Nairobi na ana nyumba moja nyumbani kwao alikowahi kuwa mbunge.
No comments:
Post a Comment