Aisee ni bonge la soo! Wanawake ambao majina yao hayakupatikana, wakazi wa Sinza, Dar es Salaam wamekumbana na sekeseke
la aina yake la ubakaji kisa kikiwa ni uvaaji wa vimini ambao kwa sasa umeshika kasi kila kona Bongo, Risasi Mchanganyiko lina
mzigo kamili.
wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya
kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.
Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta
katika hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo wakaonja joto ya jiwe.
Warembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda, walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na Morogoro, Dar.
“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,
wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.
WAJIFANYA JEURI
Mwendesha bodaboda mwingine aliliambia gazeti hili kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu
kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
MATUSI NJENJE
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba
badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama kabisa.
MWENYE ‘MDOMO MCHAFU’ AKIONA
“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’
walimkamata na kumpa kichapo kikali.
“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa
ameshachaniwachaniwa nguo na ku... (hayaandikiki gazetini),” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
BAJAJ YATUMIKA KUMUOKOA
Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia
kurudi wakiwa kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.
“Wale wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa
mwenzao na kutokomea naye kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.
ACP KENYELA ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela ambapo alipoulizwa juu
ya tukio hilo, alisema hajapata taarifa lakini aliwaasa wasichana wanaovaa nusu utupu na wote wanaojiuza kuacha mara moja.
NENO LA RISASI MCHANGANYIKO
Kukithiri kwa tabia ya kuvaa vimini kwa baadhi ya wanawake kunazidi kuchukua sura mpya sehemu mbalimbali Bongo, jambo
linalochochea maambukizi mapya ya magonjwa ya zinaa kama Ukimwi.
Ni rai yetu kuwa taasisi na mamlaka stahiki zitachukua hatua kukomesha tabia hiyo kabla ya raia kuchukua sheria mkoni, jambo
ambalo ni baya zaidi.
la aina yake la ubakaji kisa kikiwa ni uvaaji wa vimini ambao kwa sasa umeshika kasi kila kona Bongo, Risasi Mchanganyiko lina
mzigo kamili.
Mrembo akilia baada ya kunusurika kubakwa
Mwanahabari wetu akiwa katika Oparesheni ya Fichua Maovu inayoendeshwa na Magazeti ya Global Publishers, mwishoni mwa wiki iliyopita usiku wa manane, alinyetishiwa tukio la wanawake watatu kuvamiwa na midume na kufanyiwa kitu mbaya baada ya
kuchaniwa vimini vyao maeneo ya Barabara ya Shekilango, Dar kabla ya kuokolewa na wasamaria wema.
Wananchi wakiwa wamemzunguka
WAONESHA MAUNGO NYETI BILA ‘MAKUFULI’Wasichana hao, wakiwa wamejipodoa vilivyo na kutinga vimini vilivyoonesha sawia maungo yao nyeti bila ‘makufuli’, walijikuta
katika hali hiyo mbaya baada ya kurushiana maneno na vijana hao wahuni hivyo wakaonja joto ya jiwe.
Akisaidiwa kuingia katika bajaj na wasamalia wema
WATOKA SINZA KUELEKEA MANZESEWarembo hao ambao walikuwa wakitokea Sinza kuelekea Manzese, Dar walivamiwa na vijana hao ambao wengi wao ni waendesha
pikipiki maarufu kama bodaboda, walipokaribia Makutano ya Barabara ya Shekilango na Morogoro, Dar.
“Kila siku wanapita hapa wakiwa nusu utupu, sasa leo tumewakomesha, serikali inatangaza Ukimwi ni hatari, wao hawajali,
wanatutia majaribuni,” alisikika akisema mwendesha bodaboda mmoja ambaye alikuwa miongoni mwa waliowavamia wasichana
hao.
WAJIFANYA JEURI
Mwendesha bodaboda mwingine aliliambia gazeti hili kuwa waliwaeleza wasichana hao kuacha tabia ya kutembea nusu utupu
kwani ni hatari kwa maisha yao na ni kinyume cha maadili ya Watanzania lakini walijifanya jeuri ndiyo maana wakawaadabisha.
MATUSI NJENJE
Aliweka wazi kuwa baada ya kuelezwa hivyo akina dada hao hawakufurahishwa na maneno hayo na badala yake
wakawaporomoshea matusi mazito madereva hao, hali iliyowafanya wapandwe na hasira.
“Madereva wale baada ya kusikia wakitukanwa waliwavamia wasichana hao na kuanza kuwachania nguo kwa maelezo kwamba
badala ya kuwa nusu utupu, ni vema wakakaa uchi wa mnyama kabisa.
MWENYE ‘MDOMO MCHAFU’ AKIONA
“Warembo wawili walifanikiwa kutimua mbio licha ya kuchaniwa vimini vyao lakini mmoja aliyekuwa na ‘mdomo mchafu’
walimkamata na kumpa kichapo kikali.
“Shukrani ziwaendee wasamaria wema waliomukoa kwa sababu kwa vyovyote lazima angebakwa kwani alikuwa
ameshachaniwachaniwa nguo na ku... (hayaandikiki gazetini),” alisema shuhuda mmoja aliyeomba hifadhi ya jina lake.
BAJAJ YATUMIKA KUMUOKOA
Shuhuda huyo aliongeza kuwa binti huyo alifanyiwa kitu mbaya kwa kushikwa sehemu nyeti kabla ya wale wenzake waliokimbia
kurudi wakiwa kwenye Bajaj na mabaunsa wao kisha kutokomea na mwenzao aliyekuwa amehenyeshwa vya kutosha na wanaume
hao.
“Wale wasichana wawili walirudi wakiwa na Bajaj na mabaunsa, wakasaidiwa na raia wema ndipo wakafanikiwa kumuokoa
mwenzao na kutokomea naye kusikojulikana,” alisema shuhuda huyo.
ACP KENYELA ANASEMAJE?
Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Kamanda Mkuu wa Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, ACP Charles Kenyela ambapo alipoulizwa juu
ya tukio hilo, alisema hajapata taarifa lakini aliwaasa wasichana wanaovaa nusu utupu na wote wanaojiuza kuacha mara moja.
NENO LA RISASI MCHANGANYIKO
Kukithiri kwa tabia ya kuvaa vimini kwa baadhi ya wanawake kunazidi kuchukua sura mpya sehemu mbalimbali Bongo, jambo
linalochochea maambukizi mapya ya magonjwa ya zinaa kama Ukimwi.
Ni rai yetu kuwa taasisi na mamlaka stahiki zitachukua hatua kukomesha tabia hiyo kabla ya raia kuchukua sheria mkoni, jambo
ambalo ni baya zaidi.
SOURCE GAZETI LA RISASI
No comments:
Post a Comment