BIBI MWAJUMA MPONI AKIWA HOI MARA BAADA YA KUGONGWA NA GARI LA MAJI
WAZEE
WANAOSADIIWA KUWA NI WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA
POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI SHIJA NKWABI (80) NA MWAJUMA MPONI (65).
Bibi huyo
baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika vibaraza
vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea kulala
chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
Kwa
mujibu wa madreva wanaopaki magari yao eneo hilo wameiambia blog hii
kuwa hata wao walishawahi kumkosa kumgonga mara nyingi katika eneo hilo.
MATUKIO KATIKA PICHA
ASKARI WA USALAMA BARABARANI WAKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA.
BIBI MWAJUMA AKIWA HOI BAADA YA KUKANYANGWA NA GARI
AISEEE INASIKITISHA SANA
MGUU WA KULIA WA BIBI HUYO UKIWA UMEKATIKA KABISA NA KUSHIKILIWA NA NGOZI TU
VIJANA WA KAHAMA MJINI WAKIWASADIA POLISI KUUPAKIA MWILI HUO KWENYE GARI.
BIBI MWAJUMA AKITEREMSHWA HOSPITALINI.
HAPA
VIJANA WA KAHAMA WAKIMSUKUMA BIBI HUYO KUMUINGIZA HOSPITALINI ,TAFADHALI
USINIULIZE MANESI NA MADAKTARI WALIKUWA WAPI KUTEKELEZA JUKUMU LAO.
VIJANA
WAKIENDELEA KUJITOLEA KUMSAIDIA BIBI HUYO ILI AWAHI KUPATA
MATIBABU,SWALI LANGU NI JE WANA UZOEFU WA KUSUKUMA WAGONJWA KATIKA
MAGARI HAYO?
KAHAMA
Bibi
mmoja aliyefahamika kwa jina la Mwajuma Mponi anayekadiriwa kuwa na
umri kati ya miaka 75 hadi 80 amefariki dunia leo baada ya kukanyagwa na
gari la maji taka wilayani Kahama, mkoani Shinyanga.
Kwa
mujibu wa mkuu wa polisi wilayani Kahama, Gerge Simba, Bibi huyo
amekanyagwa leo mchana maeneo ya nyuma ya hospitali ya wilaya hiyo
wakati akiwa amelala chini ya gari hilo kwa ajili ya kivuli.
Simba
amesema Bi Mwajuma amefariki dunia mida ya saa moja jioni leo wakati
akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Kahama kutokana
majeraha makubwa yaliyompata ikiwemo kuvunjika vibaya mguu wake wa
kulia.
Hata
hivyo Simba ametoa wito kwa madereva kuwa makini na kuhakikisha
wanakagua chini magari yao sehemu wanapopaki au kupiga honi kabla ya
kuondoka kwani ni hatari kwa wazee wanaokuwa wanajizuia jua na hata kwa
watu wengine.
Amesema
dereva wa gari hilo ambaye alikimbia kufuatia tukio hilo, kwa sasa
anashikiliwa na polisi kwa mahojiano baada ya kukamatwa jioni hii maeneo
ya Kahama mjini.
Kumbukumbu
zimebaini kuwa Bibi huyo ni mmoja kati ya wale walioanguka April 3
katika kata ya Mhongolo wilayani Kahama na kupelekwa polisi kwa
kudhaniwa kuwa ni wachawi.
Bibi
huyo baada ya kuachiwa toka kituo cha Polisi alikuwa analala katika
vibaraza vya maduka mjini kahama wakati wa usiku na mchana hupendelea
kulala chini ya miti au chini ya magari yaliyopaki.
Credits: Kijukuu cha bibi blog
No comments:
Post a Comment