skip to main |
skip to sidebar
BUNGE LAAHIRISHWA TENA LEO MPAKA UFUMBUZI WA GESI MTWARA UTAKAPOJULIKANA
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mh.Anna Makinda ameliahirisha tena bunge leo asubuhi ili kupisha kamati
ya uongozi ya Bunge iendelee kukutana ili kutoa maamuzi na tamko kuhusu
vurugu za Mtwara zilizojotokeza jana na kusababisha mtu mmoja kufariki
dunia na uharibifu mbalimbali kutokea ikiwemo kuchomwa moto nyumba za
viongozi wa serikali,chama cha mapinduzi na nyumba ya mwandishi wa
habari wa TBC.
Pia mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nishati na
Madini umesimamishwa kwa muda mpaka ufumbuzi wa tatizo la vurugu hizo utakapopatiwa suluhisho.
Kesho bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Afrika Mashariki itajadiliwa.
No comments:
Post a Comment