BAADA ya mwaka mmoja nje ya ulingo na
miezi miwili jela, bondia bora kabisa duniani, Mmarekani Floyd
Mayweather anarejea ulingoni usiku wa leo kwenye ukumbi wa MGM Grand,
Las Vegas.
Pambano lake la mwisho alipigana na Miguel Cotto na kushinda na leo atapambana na Robert Guerrero, ambaye mwenyewe anajiita The Ghost, yaani Mzimu katika uzito wa Welter Raundi 12.

Yuko sawa: Floyd Mayweather alionekana yuko sawa wakati wa kupimzika uzito


Utaona: Mabondia hao wakitambiana wakati wa kupima uzito

Hunitishi: Mabondia wakitunishiana vifua wakati wa kupima uzito
Pambano la Mayweather na Guerrero
litaonyeshwa live na BoxNation kupitia Sky Channel 437 na Virgin Channel
546 kuanzia saa 7.30 usiku wa leo sawa na saa 9:30 kwa saa za Tanzania.
No comments:
Post a Comment