Uongozi
wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) leo umemkaribisha rasmi Mkurugenzi
Mtendaji wao mpya, Mama Mizinga Melu. Mama Melu alikuwa Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered Zambia, ambapo aliongoza benki hiyo kwa Miaka 6 kabla kuhamia NBC.
Mizinga
si mgeni kwenye sekta ya kibenki, kwani keshashika nafasi kubwa mbali
mbali akiwa na Benki ya Standard Chartered. Nafasi hizi ni kama vile
Mkuu wa Kimataifa
wa Mashirika ya Maendeleo, Uingereza ambapo alikuwa anasimamia
maendeleo ya mikakati na utekelezaji, pamoja na kuwa Mkuu wa Taasisi za
Fedha nchini Kenya na Afrika Kusini, Kanda ya Afrika.
Mama
Melu si mgeni kwa Tanzania, kwani alishawahi kuwa Mkuu wa Hazina katika
Benki ya Standard Chartered Tanzania kati ya mwaka 2000 na 2003. Kabla
ya kushika nafasi hiyo alifanya kazi kama kaimu Mkuu wa Hazina Benki ya
Standard Chartered Uganda mwaka 1998 na Zambia mwaka 1999.
Mizinga ana Shahada ya Pili (Masters) ya usimamizi wa Biashara (MBA) kutoka Chuo cha Henley Management College (Uingereza) na ni mwanachama wa Taasisi ya wafanyakazi wa mabenki(ACIB), pamoja na sifa nyengine mbali mbali.
Akizungumzia
juu ya uteuzi huo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBCi, Dk Mussa
Assad alisema, “kuwasili Mizinga ni jambo la furaha sana kwetu kwani
amekuja wakati muafaka ambapo NBC inapitia mabadiliko mengi mazuri na
tunafuraha kuwa atakuwa sehemu ya mabadiliko haya”. Pia aliongeza” Kabla
ya kuwasili kwake, benki ilikuwa ikiongozwa na Pius Tibazarwa ambaye
ameonyesha uongozi mzuri kwa kipindi hiki na kutimiza matarajio yetu
yote, na tungependa kumshukuru kwa juhudi zake kwani ametekeleza
majukumu ya ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, juu ya jukumu la kuendesha
idara yake mwenyewe.”
Mama
Melu amepokea nafasi hiyo kutoka kwa Pius Tibazarwa ambaye alishikilia
nafasi hiyo kama Kaimu Mkurugenzi Mtendaji tangu mwanzo wa mwaka huu.
Mizinga
amepangiwa kukutana na viongozi wa serikali pamoja na wateja wakubwa
kwa ajili kutambulishwa rasmi kabla kuanza safari za kutembelea matawi
ya NBC yaliopo mikoani ili kukutana na wafanyakazi na wateja walioko
huko.
No comments:
Post a Comment