Polisi
katika Mkoa wa Rukwa likishirikiana na Polisi wa Tabora pamoja na
kikosi kazi maalumu cha kitaifa, limefanikiwa kuwatia nguvuni watu tisa
waliokuwa wakisakwa kwa muda mrefu kwa tuhuma za kumkata mkono, Mwigulu
Matonange(10) mlemavu wa ngozi Februari 15 mwaka huu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwarwanda alisema watuhumiwa hao walikuwa wakisakwa kwa muda
mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa.
mrefu kutokana na mtandao mkubwa waliokuwa nao, hatimaye baadhi wamefanikiwa kukamatwa huku wengine bado wakiendelea kutafutwa.
Aliwataja
watuhumiwa hao kuwa ni Weda Mashilimu(29),Nickon Kadogoo(25), Peter
Msabato(32),Ignas Sungura(27),Faraja Mwezimpya (31) pamoja na Kurwa
Hamis (29) wote wakiwa ni wakazi wa Kijiji ha Ilemba Rukwa.
Aliwataja
watuhumiwa wengine ambao ni Hamis Mnywanywa ambaye ni mganga wa jadi na
mkazi wa Karema Katavi,James Paskali(24) mkazi wa majimoto, pamoja na
Ibrahimu Tella(27) mkazi wa kijiji Masanula-Usule Shinyanga.
Kamanda
alisema kukamatwa kwa watuhumiwa hao kulifuatia uchunguzi wa kina
uliokua unafanywa na polisi hao kupitia mawasiliano ya simu na taarifa
mbalimbali za kipelelezi ambapo siku ya April 22 walifanikiwa kumnasa
Nickon Kadogoo akiwa Katavi na mkono huo akiupeleka mkoani Tabora ambapo
angepata soko.
Baada
ya kuhojiwa mtuhumiwa huyo alidai kuwa yeye na wenzake hao waliagizwa
mkono huo na mganga wa jadi aitwaye Rashid Manywanywa, ambapo aliwaahidi
angemlipa kila mmoja Sh600 milioni kama wangempelekea mkono huo.
Alisema
baada ya tukio la kumkata mtoto huyo mkono na kumpelekea mganga huyo
alidai kuwa hana fedha zote hizo kwani wao walishindwa kutumia akili kwa
kuwa hata yeye ni maskini angelipata wapi fedha zote hizo, hivyo hawezi
kununua mkono huo.
Baada
ya kuona soko limeshindikana ndipo walipoamua kufanya mawasiliano na
watu wengine na kuhakikishiwa katika Mikoa ya Tabora na Shinyanga kuna
soko la uhakika ndipo safari ya kuelekea huko ikaanza.
Kwa
upande wake, mganga huyo wa jadi alikiri kuwaagiza watuhumiwa hao mkono
huo na kudai kuwa alitaka kutumia kutengenezea chombo cha usafiri
ambacho alidai kuwa ni ungo ambao unatumika na wachawi kusafiria nyakati
za usiku.
No comments:
Post a Comment