Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, June 10, 2013

Geita Gold Mine yatoa Msaada kupambana na Ukimwi nchini.


 

IMG_9875
 
 Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani akiwatambulisha watoto yatima Irene Joachim Katikati na Geofrey Yohana watakaopanda mlima Kilimanjaro katika kuhamasisha taasisi na mashirika mbalimbali kuchangia fedha kwa ajili ya mapambano dhidi ya VVU na Ukimwi nchini Tanzania hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine.
IMG_9893
Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma Mrisho, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar Issa wakimkabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 15,000,000 Sister Adalbera Mukure wa Mkurugenzi wa Kituo cha Kulelea watoto yatima cha Moyo wa Huruma cha Geita wakati wa hafla maalum ya kukabidhi fedha hizo kwa mashirika mablimbali yanayopambana na ugonjwa wa ukimwi iliyofanyika Ijumaa kwenye hoteli ya Hyatt Kilimanjaro jijini Dar es salaam fedha hizo zinakusanywa Mgodi wa Dhahabu ya Geita Gold Mine na washirika wake kwa kupanda mlima Kilimanjaro.
IMG_9903
 Kutoka kushoto ni  Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Geita Gold Mine Omar Issa, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya Kampuni ya bia ya Serengeti Mzee Mark Bomani na Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi TACAIDS Fatma Mrisho,  wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa TACAIDS kutoka kulia ni Jumanne Issango  Mkurugenzi wa Uraghibishi, Beng’i Issa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala na Moriss Lekule Mkurugenzi wa Mwitikio wa Taifa hafla hii ilifadhiliwa na Geita Gold Mine

No comments:

Post a Comment