Habari zilizotufikia hivi punde bomu limelipuka katika eneo la Soweto mkoani Arusha kwenye mkutano wa Chadema leo, na kusababisha watu wanne kufariki Dunia.
Mlipuko
huo umetokea majira ya saa 12:00 na majeruhi ni zaidi ya 10
wamekimbizwa katika Hospitali ya Mount Meru STK 8493 kwa matibabu zaidi.
Bomu hilo ambalo lilikuwa limetegewa katika mkutano huo lilipuka na kusababisha mauti na kujeruhi watu zaidi 10.
Pia gari limevunjwa vioo na wananchi kwa madai ya kwamba limeshindwa kuokoa maisha ya majeruhi.
Inaonekana bomu lilitegwa karibu na gari la matangazo, Mtoto aliyelipukiwa na bomu amefariki uwanjani.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Abbas amesema kwamba watu wawili ndio wamepoteza maisha.
No comments:
Post a Comment