Kwa
mara ya pili mfululizo, jiji la Mbeya litakuwa mwenyeji wa ligi kuu ya
Netiboli taifa ambapo naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Philip Mulugo anatarijiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi kuanzia
Agosti 24 hadi Septemba 7.
Mwenyekiti
wa chama cha Netiboli Mkoa wa Mbeya, Mary Mung’ong’o ameumabia mtandao
huu kuwa ligi hiyo inafanyika kwa mara nyingine kutokana na ombi la
Waziri Mulugo kwa vile ligi hiyo haikuwa imefana, hivyo akaiomba CHANETA
kuwapa Mbeya fursa nyingine ya uwenyeji.
Alisema
maandalizi ya ligi yameanza na kusema zinahitajika sh milioni 16
kufanikisha na kuongeza kuwa hadi sasa, hawajajua timu ngapi zitashiriki
kutokana na jukumu hilo kuwa chini ya Chama cha Netiboli Tanzania
(CHANETA).
Hata
hivyo, mwenyekiti huyo alitoa wito kwa viongozi wa ngazi mbalimbli
wakiwemo wadau wenye mapenzi na mchezo kutoka mkoani hapa kujitoa kwa
hali na mali kuyafanikisha ili yawe chachu ya kukua kwa mchezo huo
nchini kwa maslahi ya vijana na taifa.
Aidha, mwenyekiti huyo alitamtambulisha Nwaka Mwakisu kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano hayo.
Akizungumzia
mashindano hayo, Mwakisu alisema ni fursa kwa watu wa Mbeya kujitangaza
kibiashara kupitia mchezo huo na kufuta makosa yaliyofanyika mwaka
jana.
Alisema
katika kufakisha mashindano hayo, nguvu ya pamoja inahitajika kuanzia
viongozi wa kisiasa, serikari na vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment