Mimi binafsi nilikuwepo eneo la tukio na nilikua takriban mt 8 na lilipotua Bomu baada ya kurushwa.
Ilikua ni mida ya saa 11:50. Mwenyekiti Mbowe alishuka kwenda kukusanya pesa(SADAKA) kwa ajili ya Kugaramia chakula na vinywaji kwa mawakala siku inayofuatia ambayo ndio siku ya Uchaguzi.
Mara tu Mbowe aliposhuka Bomu likarushwa kutokea MASHARIKI KASKAZINI mwa uwanja kuelekea alipokuwa Mbowe akikusanya pesa.
Mimi nilikuwepo takriban mt 9 kwa upande wa Mashariki na ilipoanguka Bomu.Kwa wale wanaojua Jiografia ya Uwanja wa Soweto Jukwaa kuu lilikua upande wa Mashariki mwa uwanja likiangalia Mgharibi kulikokua wamekaa watu.. Na nyuma ya Jukwaa (GARI LA MATANGAZO) ni barabara na ngambo ya barabara ni Nyumba(Kotaz) za AICC. mbele ya nyumba hizo kuna KICHAKA cha Maua ya Bogavilia.
Bomu liliporushwa lilpita juu yetu likiwa limefungwa na kitu cheusi kama Soksi au Nailoni.Hakika binafsi kabla ya bomu hilo kutua chini na kulipuka nilipoona ikipita juu nilidhani ni Popo alietoka kwenye mti uliopo Jirani na Jukwaa kwa upande wa mashariki mwa uwanja.
Polisi walikuepo uwanjani upande wa Kusini magharibi mwa uwanja na jukwaa kuu.! Bomu lilipo lipuka yaonekana kabisa Mrusha bomu alikua kajificha kwenye kichaka cha Maua ya bogavilia ngambo ya barabara Mashariki mwa Uwanja nyuma ya Jukwaa kuu ndio maana hakuweza kuonekana.
KILICHOTOKEA KATI YA POLISI NA RAIA:
Baada ya Mlipuko na watu kuanza kukimbia huku na kule ndipo Polisi bila kujua nini kilichotokea kwa kua walikua mbali wakadhani watu wanawakimbiza wao. Muda huo tayari watu wachache walikua chini wakiwa wamejeruhiwa na BOMU na Polisi nao walikua kwanza ndio wamezunguka kuja upande wa Mashariki mwa uwanja kulipotokea Mlipuko.
Lakini kwa bahati mbaya Watu wengi na Polisi haswa waliokua mbali hawakujua kwamba mlipuko huo ni wa Bomu. Wengi walijua ni bomu la Machozi limerushwa na Polisi.
Pale ndipo Watu wakawa wanawafuata Polisi na polisi nao wakaanza kurusha risasi hovyo kuelekea jukwaa kuu na baadhi ya risasi kupiga watu na zingine kutoboa tanki la mafuta ya Lori la matangazo ambalo ndilo lilikua Jukwaa kuu.watu wengi walijeruhiwa na Risasi zilizokua zikirushwa na polisi na sio bomu.
Baada ya hapo ndipo watu wakaanza kuwarushia polisi mawe na muda huo tangia bomu kurushwa ni zaidi ya dk 7 au 10.
Polisi baada ya kuzidiwa nguvu walikimbia ndipo watu wakaanza kuwachukua majeruhi kuwapeleka Hospitali. Polisi walirudi baadae baada ya kama dk 45 wakati hali ikiwa imetulia.
Huu ndio ukweli na mh LUKUVI kudanganya kuwa eti watu wa CDM ndio walimtorosha mtuhumiwa sio za kweli.ni za uongo na za KUPOTOSHA UMMA.
Uongozi wa JF Naomba msiunganishe mada hii na nyingine. Ijitegemee.source jamii forum
Monday, June 17, 2013
LUKUVI na wengineo, Huu ndio ukweli jinsi Bomu lilivyorushwa. Mengine ni PROPAGANDA!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment