Alen Pamic
ZAGREB, Croatia
Hivi karibuni, Pamic
alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari,
ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku
madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo
NYOTA wa soka la
kulipwa raia wa Croatia, Alen Pamic ameanguka uwanjani na kufariki dunia wakati
wa mechi ndogo isiyo ya kimashindano, gazeti la kila siku la Vecernji List
limesema katika toleo lake mtandaoni la leo Jumamosi.
Taarifa hiyo
imeripotiwa kwa ufupi, huku ikiwa haina maelezo zaidi kuhusiana na kifo cha
Pamic aliyekufa akiwa na umri wa miaka 23 tu.
Pamic, aliyekuwa
akichezea klabu ya NK Istra 1961 katika ligi ya daraja la juu zaidi nchini
hapa, alikuwa na historia ya matatizo ya moyo, ambayo yalimwangusha dimbani
mara tatu kabla ya tukio hilo lililochukua uhai wake.
Hivi karibuni, Pamic
alipoteza fahamu katika mechi ya ligi dhidi ya Lokomotiva iliyopigwa Februari,
ambapo licha ya matatizo yake hayo alisisitiza kuendelea kucheza soka, huku
madaktari wake wakimruhusu kufanya hivyo.
Pamic aliyekuwa
kiungo mahiri dimbani, aliutumia msimu mmoja wa 2010/11 kuchezea klabu ya
Standard Liege ya Ligi Kuu ya Ubelgiji, lakini klabu hiyo ikamtema muda mfupi
baada ya kupata shambulio la moyo na kuzimia akiwa mazoezini, gazeti la
Vecernji limesema katika taarifa yake.
Pamic ni mtoto wa
nyota wa zamani wa kimataifa wa Croatia, Igor Pamic, ambaye kwa sasa anainoa
klabu ya NK Istra 1961 aliyokuwa akiichezea marehemu.
Supersport.com
Alen Pamic aliyelala, akipatiwa huduma ya kwanza na wachezaji wenzake katika moja ya mechi alizowahi kuzimia uwanjani hivi karibuni kutokana na matatizo ya moyo
No comments:
Post a Comment