Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Mwenyekiti
wa klabu ya Wigan Athletic, Dave Whelan amethibitisha kuwa wiki ijayo
anaanza usaili wa kupata makocha wa kuifundisha klabu hiyo na kusema
kuwa muda kama huu wiki ijayo tayari timu hiyo itakuwa na kocha mpya.
Whelan
amelazimika kutafuta meneja mpya baada ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo
Roberto Martinez kutimkia katika klabu ya Everton kurithi mikoba ya
aliyekuwa kocha wa klabu hiyo David Moyes aliyejiunga na mabingwa wa
ligi kuu nchini England, Manchester United.
Whelan
ameuambia mtandao wa michezo wa Sky Sports kuwa amepata makocha 10 hadi
12 wa kuwafanyia usaili siku chache zijazo na wiki ijayo atatangaza
rasmi kocha mpya wa mabingwa hao wa kombe la FA.
“Kuna maombi 50, lakini siwezi kuwafanyia usaili yote, ila nawashukuru kwa kutuma maombi”. Alisema Whelan.
Majina yanayotaja kuziba nafasi hiyo ni
Brighton’s Gus Poyet, Mike Phelan na Rene Meulensteen – wote walikuwa
wasaidizi wa Ferguson, Karl Robinson na kocha wa zamani wa Bolton na
Burnley, Owen Coyle.
Hata
hivyo Whelan alisema hataangalia majina, lakini atazungumza na makocha
wengi na mwishoni anataka kumsainisha kocha mkubwa na haitakuwa kazi
nyepesi kwake.
Nafasi imebaki wazi Wigan: Roberto Martinez (kulia) ametimka Wigan na kujiunga na Everton ili kurithi mikoba ya David Moyes
Katimka baada ya kuacha taji: Martinez ametimka baada ya kushinda taji la FA
Kocha wa zamani wa Manchester United Rene Meulensteen (kushoto) naye ametajwa kuwania kibarua katika klabu ya Wigan
source fullshangwe blog
No comments:
Post a Comment