Hatua hiyo ya Kampuni ya Startimes kuondoa Star Tv kwenye orodha ya vituo vinavyopatikana kwenye king’amuzi chake ilianza juzi.
Startimes ilianza kutoa taarifa kuwa
kutokana na matakwa ya Star Tv, wameamua kuitoa kwenye orodha ya chaneli
zao bila ya ufafanuzi wa kina kuhusu uamuzi huo.
Waziri wa Sayansi, Mawasiliano na
Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alipotafutwa kutolea ufafanuzi wa
kitendo hicho, alisema hafahamu lolote.
“Sifahamu kwani niko Pemba lakini labda
watafute Mamlaka ya Mawasilino Tanzania (TCRA), Profesa John Nkoma
(Mkurugenzi wa TCRA) watakuwa wanajua,” alisema Profesa Mbarawa.
Profesa Nkoma hakupatikana jana na juhudi
za gazeti hili zilifanikiwa kumpata Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent
Mungi aliyesema hafahamu sababu za Startimes kuitoa Star Tv katika
kurusha matangazo ya dijitali.
“Kulikuwa na matatizo ya makubaliano baina
ya pande hizo mbili, Star Tv walilalamika jinsi ya kuonekana kwa chaneli
yao kwa mtoa huduma,” alisema Mungi.
Mungi alisema kwa mujibu wa leseni ya
kurusha matangazo ya kimataifa, Star Tv inatakiwa kuonekana katika
dijitali zote za ndani na uamuzi waliochukua unakiuka makubaliano hayo.
“Hata kama kulikuwa na matatizo, hawakutakiwa kuchukua uamuzi huo, kwani
wangekutana na mamlaka husika (TCRA) na kusikiliza malalamiko hayo
kisha kuwasuluhisha na tatizo hilo likamaliza,” alisema Mungi.
Mwananchi
No comments:
Post a Comment