Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Emmanuel John Nchimbi(Mb) atakuwa
Mgeni Rasmi katika ufungaji wa Mafunzo ya Uongozi Ngazi ya Juu kwa
Maafisa Magereza(Gazetted Officer's Course) yatakayofanyika tarehe 12
Juni, 2013 saa 6:00 mchana katika Chuo cha Maafisa Magereza Ukonga
kilichopo Manispaa ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
Mafunzo hayo ya Uongozi Ngazi ya Juu yalianza tarehe 03 Mei, 2013 yana jumla ya Maafisa 244 ambapo wanaume ni 201 na wanawake 43. Kati yao wapo wanafunzi 10 kutoka Vyuo vya Mafunzo Zanzibar.
Ratiba kamili ya Mgeni Rasmi katika shughuli hiyo itajumuisha mambo yafuatayo; i) Kukagua Gwaride Maalum lililoandaliwa na wahitimu hao;

ii) Kutoa vyeti kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika Mafunzo ya darasani na Mafunzo ya
mbinu za medani;
iii) Kuvisha cheo cha Mrakibu Msaidizi wa Magereza kwa mhitimu mmoja kwa niaba ya wahitimu 244 wa Mafunzo hayo;
iv) Kupata maelezo Maalum kutoka kwa Kamishna Jenerali wa Magereza na kumkaribisha Mgeni Mgeni Rasmi kuhutubia na;
v) Mgeni Rasmi kuhutubia na kufunga Mafunzo hayo.
Vyombo vya habari vinakaribishwa pamoja na Wananchi kwenye hafla hiyo siku na muda uliopangwa.
Imetolewa na;
Lucas Mboje -
INSP, Afisa Habari wa Jeshi la Magereza.
No comments:
Post a Comment