Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 12, 2013

HAFLA YA KUWAKARIBISHA MAKAMISHNA WAKUU WA MAGEREZA TOKA JUMUIYA YA MAENDELEO NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA ZA FANA JIJINI DSM


photoKamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(Suti nyeusi) akiwa na Makamishna Wakuu wa Magereza kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika katika hafla fupi aliyowaandalia baada ya kumaliza Kikao cha Mawaziri wanaohusika na Ulinzi na Usalama toka Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika( wa kwanza kushoto ni Kamishna Mkuu wa Magereza wa Zambia, Percy Chato, ( wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Magereza wa Msumbiji, Dkt. Eduardo Sebastiao, (wa tatu kushoto) ni Kamishna Mkuu wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Tom Moyane, (wa kwanza kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Malawi, Naibu Kamishna wa Magereza, Ms. Phiri, ( wa pili toka kulia) ni Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Namibia, Kamishna wa Magereza, Ms. Feris. Hafla hiyo ilifanyikia katika Viwanja vya Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga, Dar es Salaam( Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).photo (2)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akitoa hotuba fupi wakati wa hafla aliyowaandalia Makamishna Wakuu wa Magereza Nchini toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika. Hafla hiyo imefanyikia katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)photo (1)Mwakilishi wa Kamishna Mkuu wa Magereza Nchini Namibia, Bi. Feris akitoa neno la shukrani kwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja(Suti nyeusi)kwa kuwaandalia hafla hiyo fupi pamoja na kupata fursa ya kubadilishana mawazo ya namna ya Uendeshaji wa Magereza. Hafla hiyo imefanyikia katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).photo (3)Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja ( suti nyeusi)akimkabidhi Zawadi ya Kikapu Kamishna Mkuu wa Magereza wa Zambia, Percy Chato. Kikapu hicho kimetengenezwa na Wafungwa wa Gereza Kuu Ukonga.  Hafla  fupi ya kuwakaribisha Wakuu wa Magereza Nchini toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika imefanyikia katika Bustani ya Kikosi Maalum cha Kutuliza Ghasia Magerezani, Ukonga Dar es Salaam(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).photo (4)Kikundi cha Sarakasi kinachoundwa na Askari wa Jeshi la Magereza wakionesha umahiri wao katika hafla ya kuwakaribisha kama unavyoweza kumuona Askari wa Kike ambaye alikonga nyoyo za Makamishna Wakuu wa Magereza toka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika hawapo pichani(Picha na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

No comments:

Post a Comment