Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, July 11, 2013

MAAJABU::KUTANA NA FAMASI YENYE GENGE NA JIKO NDANI


Muonekano wa ndani ya duka hilo.

Mwaija Salum na Chande Abdallah
HII kali! Oparesheni Fichua Maovu a.k.a OFM inazidi kufukunyua vya kufukunyuka, safari hii ikikutana na kioja cha aina yake ambapo ilinasa duka la kuuza dawa za binadamu ‘pharmacy’ likifanya biashara nyingine tofauti na hiyo.
Mnyetishaji wetu ambaye hakupenda jina lake liandikwe, alitonya kuwa duka hilo linapatikana Hananasif, Kinondoni, Dar es Salaam.

Timu ya OFM ilivamia eneo hilo na kujiridhisha ambapo ilishuhudia bidhaa nyingine kama mbogamboga, nazi, ndizi, vitunguu, nyanya na mazagazaga mengine rafiki kwa mama yakiuzwa ndani ya duka hilo.
Cha kushangaza zaidi, pia ndani ya duka hilo la kuuzia dawa muhimu, kulikuwa na jiko la kupikia likiendelea kutekeleza majukumu ya kukaangiza kama kawaida. NA GLOBAL PUBLISHER


Mariam Seleman ambaye ni mmiliki wa duka hilo.

Timu yetu ilifunga safari hadi kwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Hananasif, Suleiman Lada na kumweleza juu ya tukio hilo ambapo iliungana naye hadi dukani hapo na kujionea jambo lililomshangaza na kusema: “Sikufahamu kabisa kama kuna kitu kama hiki mtaani kwangu.

“Lakini nitafuatilia hili suala kisheria nione, lazima afuate taratibu zilizowekwa na wizara (ya afya) katika kuuza dawa za binadamu, vinginevyo hili duka nitalifunga.”

Baadhi ya bidhaa zilizopo katika duka hilo.

Muuzaji wa duka hilo ambaye ndiye mmiliki aitwaye Mariam Seleman, alisema hajui kama kuna sheria inambana kutochanganya biashara hiyo na mahitaji mengine.

“Kiukweli mimi nilikuwa sijui kama ni kosa kufanya hivyo ndiyo maana nimeuza hapa kwa mwaka mzima na sijawahi kuulizwa na mtu yeyote. Hata hivyo kwa sababu leo mmenielewesha basi itabidi nichague biashara moja ya kufanya kama ni dawa au vyakula,” alisema Mariam.




No comments:

Post a Comment