Dawa za kulevya.
Huku
akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya
kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’
amepata balaa jipya.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na
mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo
wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari
zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba
wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo
ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku
Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo
lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine
vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo,
wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.
“Hicho
ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye
mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka,
wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma
kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria
ikafuata mkondo wake.
“Hii
inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na
kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa,
ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea
maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.
MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya
kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza
picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya
kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si
mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati
baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande
hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.
WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya
staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania
waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo
la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa
kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa
kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa
dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania
mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.
POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari
kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi
hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo,
Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani
ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija
mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari
lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea
kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza
majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye
nyumba ya Masogange.
“Julai 20
alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo
mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika
mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo
maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna
kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja
kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,”
kilisema chanzo.
KUMBUKUMBU
Julai 5,
mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika
Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita.
-GPL
No comments:
Post a Comment