Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akimsaidia kutembea mtoto, Asante Mtega wa kituo
cha kulea na kuwasaidia watoto wenye ulemavu cha cha Inuka kilichopo
Mayale Iringa wakati alipokitembelea Julai 8,2013. Katikati ni Mkewe
Tunu na Kushoto ni Askofu wa kanisa Katoliki Njombe, Alfred Maluma.
(picha na Ofisiya Waziri mkuu).
Waziri
mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Igwachanya
wilayani Wanging’ombe wakati alipoingia kijijini hapo akiwa katika
ziara ya mkoa wa Njombe Julai 8, 2013. Kushoto ni Mkewe Tunu na Kulia ni
mkuu wa Wilaya hiyo Estelina Kilasi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Askofu wa Jimbo Katoliki la Njombe, Alfred
Maluma wakiweka jiwe la msingi la Chuuo cha Kilimo na Mifugo cha Mare-
Mayale , Katika wilaya ya Wanging’ombe. Jana. kulia ni mkewe Tunu
Pinda.
Waziri
mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Askofu wa Jimbo Katoliki la
Njombe,Alfred Maluma kabla ya kuwaslimia wananchi katika misheni ya
Ilembula wilayani Wanging’ombe akiwa katika ziara ya mkoa wa Njombe
leo.
No comments:
Post a Comment