Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, July 30, 2013

Nayemar afanyiwa vipimo Barca

neyman 53eca
Neymar akifanyiwa vipimo (HM)

MCHEZAJI aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 50, Neymar amefanyiwa vipimo vya afya mjini Barcelona tayari kwa mazoezi yake ya kwanza na klabu yake hiyo mpya.

Barcelona itawapokea tena wachezaji wote waliokuwa kwenye Kombe la Mabara leo mcha, na Neymar atakuwa miongoni mwao pamoja na akina Xavi, Andres Iniesta, Cesc Fabregas na Lionel Messi.

Itakuwa nafasi yake ya kwanza kujaribu kuwavutia wachezaji wenzake wapya baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa pili ghali katika klabu hiyo nyuma ya Zlatan Ibrahimovic aliyesajiliwa mwaka 2009 kwa Pauni Milioni 56.
Neymar aling'ara kikosini Brazil na kuiwezesha kutwaa Kombe la Mabara Juni mwaka huu akiwafunga wachezaji wenzake wengi wa Barca wanaounda kikosi cha Hispania.
Mmoja wa wapinzani wake siku hiyo, Fabregas, bado anatakiwa na Manchester United na kocha David Moyes anatumai kumnasa kabla ya pazia la usajili kufungwa Septemba.

No comments:

Post a Comment