Na Musa MatejaTHE big boss wa The Endless Fame Production, Wema Isaac Sepetu ametundika mtandaoni picha zinazoonesha mapaja yake jinsi yalivyoharibika na kuweka michirizi ambapo alipoulizwa na shushushu wetu kulikoni, alisema kuwa hataacha mkorogo hadi maduka yafungwe.
Baadhi ya marafiki zake walianza kujadili namna alivyoharibika na wengine kudai matumizi ya vipodozi vikali maarufu kwa jina la mkorogo ndiyo vimemfanya apasuke kiasi hicho.
Wema,
baada ya kupokea maoni mengi juu ya picha hizo mengine yakiwa ni ya
kejeli, aliwajibu kwa kuandika kuwa hataacha matumizi ya mkorogo hadi
maduka yanayouza yafungwe.Wema alipotafutwa na gazeti hili ili aweze kuweka wazi madai haya hakutoa ushirikiano kufuatia simu yake ya kiganjani kuita muda wote bila kupokelewa.Habari na GPL




No comments:
Post a Comment