Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 22, 2013

ALIYEBAMBWA NA DAWA ZA KULEVYA 'AIRPORT' DAR APANDISHWA KIZIMBANI.



Edwin Monyo.
Mtuhumiwa  Edwin Monyo (39) anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya zenye thamani ya Sh milioni 68, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka hayo.

Monyo alifikishwa mahakamani hapo jana na kurudishwa rumande, kwa kuwa mashitaka  yanayomkabili, hayana dhamana. Alisomewa mashitaka mawili na Wakili wa Serikali, Leonard Chalo mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa.

Wakili Chalo alidai Agosti 14 mwaka huu katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, Monyo alikamatwa akisafirisha gramu 1,512.65 za dawa za kulevya aina ya heroin. Alidai siku hiyo hiyo alikamatwa akiwa na gramu 3,477 za dawa hizo aina ya bangi.
Mshitakiwa hakuruhusiwa kujibu mashitaka ya kukutwa na dawa za kulevya, kwa kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kuisikiliza. Kesi itatajwa Septemba 3 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment