



Na Kibada Kibada- Mbeya,
Maonesho
ya Nanenane leo yameingia siku ya Pili tangu ylipofunguliwa na Waziri
wa Uchukuzi Dr Halson Mwakyembe Jijijini Mbeya ambayo yameonekana kuwa
kivutio kikubwa kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya nyanda za juu na wale
wananchi wakutoka mikoa ya jirani na kanda hii hasa kutoka nchi jirani
zaMalawi na Zambia ambao nao wamejumuika kuonesha bidhaa zao .
Baadhi
ya wakulima wakizungumzia hali ya maoneshao wamelezea kufurahishwa na
umahili wa waoneshaji wakulima kuwa wamekuwa na umahili wa hali ya juu
katika kubuni bidhaa za kilimo na mifugo, na kusema kuwa elimu hii
inatakiwa kufika hadi vijiji pindi watoka katika maonesho hayo wapeleke
ujuzi huo kuendeleza kule kwa wakulima.
Washiriki
wengi wamekuwa wakimminika kuja kujifunza kwenye banda la Halmashauri
ya wilaya ya mpanda ambalo limesheheni kila aina ya bidhaa za ndani na
nje ya mabanda wakivutiwa na maelezo yanayotolwa na wataalam na wakulima
na kivutio kikubwa ikiwa ni gazeti la mpandaleo lililosheheni habari za
mkulima na elimu ya kilimo bora na cha kisasa ambapo waoneshaji
wamekuwa wakiyapigania magazeti hayo yanayogawiwa bora ili kutoa elimu
ya kilimo bora na kuhabarisha wakulima.
No comments:
Post a Comment