Bodi ya taifa ya Miss
Tourism Tanzania Organisation (MTTO), yenye dhima ya kikomo ya kuratibu
na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania, imetangaza kusimamisha
kufanyika mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014 kwa
lengo la kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa
mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo Erasto Gideon Chipungahelo, amesema uamuzi huo mgumu umechukuliwa katika kikao cha bodi hiyo kilicho fanya tathimini ya miaka mitano ya Miss Utalii Tanzania. Mashindano ya Miss Utalii Tanzania yalifanyika mara ya kwanza nchini Mwaka 2004 jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee na Fainali za Tano zilifanyika Mei 2013, jijini Tanga katika Uwanja wa Mkwakwani.
Bodi katika tathimini hiyo imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo, utendaji na hujuma. Bodi pia imebaini changamoto mbalimbali ambazo zinapelekea sanaa ya urembo kudumaa au kuto kua kwa kasi inayo takiwa ukilinganisha na nchi jirani na hata nyinginezo Duniani.
Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na mfumo wa upatikanaji wadhamini, ambao umepelekea wabunifu wengi wa kazi za sanaa kukwama kwa kukosa wadhamini, changamoto nyingine ni hujuma za baina ya waandaaji, washiriki na hata wadhamini ambako kumepelekea kuwa na washiriki na viongozi mamluki wanao pandikizwa katika mshindano kwa lengo la kuchafua na kudhoofisha mashindano mengine.
Changamoto za udhamini na hujuma, zimekuwa ni tatizo kubwa kwa mashindano haya tangu kuanzishwa kwake ambapo kwa nyakati tofauti propaganda chafu dhidi ya shndan na viongozi zimekuwa zikienezwa kwa njia mbalimbali,majaribio mbalimbali ya wazi na mafichoni ya kupora shindano au hata kujeruhi viongozi.Hatua iliyo fikia hta kuporwa wadhamini waliojitokeza .
Licha ya ukweli kuwa katika umri wake wa miaka Miss Utalii Tanzania ndilo shindano lenye mafanikio makubwa zaidi kitaifa na kimataifa kuliko mashindano mengine yoyote nchini na hata Afrika mashariki na kati.

No comments:
Post a Comment