CHAMA Cha
Mapinduzi (CCM) kimeisambaratisha ngome ya CHADEMA mjini hapa baada ya wanachama
wake 365 wakiongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa na Mjumbe wa Baraza
Kuu la Vijana la chama hicho (BAVICHA), Frank Fumpa.
Wanachama hao walipokewa na Mwenyekiti wa Umoja wa
Wazazi Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM , Abdallah Bulembo
wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika Nzovwe Sokoni mjini hapa.
Wengine waliohamia CCM na kurejesha kadi zao kwa
Bulembo wakati wa mkutano huo ni wapiga debe maarufu wa chama hicho mjini hapa,
Alex Mwaisango na Ambundwile Mwantondo.
Wanachama hao wa CHADEMA waliohamia CCM wakati wa
mkutano huo na kupokewa na Bulembo ni miongoni mwa wanachama 375 kutoka vyama
vya upinzani wakiwemo wanne kutoka CUF na sita kutoka TLP.
Katika mkutano huo pia Bulembo alikabidhi kadi kwa
wanachama wapya wa CCM 279 wakiwemo vijana 15 waendesha pikipiki (Bodaboda),
Umoja wa Wazazi Tanzania 15 na Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wanachama
15.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake sababu za kuodoka
CHADEMA na kuhamia CCM, Fumpa alisema baada ya kutafakari kwa kina kwa muda
mrefu walipokuwa ndani ya chama hicho wamegundua hakina mpango wa kuwatetea na
kuwaletea maendeleo Watanzania zaidi ya kupanikiza chuki na uhasaba kwa wananchi
dhidi ya serikali yao.
Fumpa alisema wakiwa ndani ya chama hicho wameshuhudia
mengi ikiwemo msimamo wa viongozi wa chama hicho wa kuwatumia wanachama hususan
vijana wa chama hicho kuongoza vurugu na kutokana na vurugu hizo katika baadhi
ya maeneo zimesababisha vifo vya watu wasio na hatia.
Alisema wameamua kurejea CCM kwa umamuzi wao bila
kushawishiwa na yeyote baada ya kubaini wanapoteza muda mure wa kushiriiana na
Watanzania wengine kuharakisha maendeleo yao na kuwashauri warejee CCM kwenye
matumaini ya kweli ya ufumbuzi wa changamoto zinazowakabili.
"Zipo kauli za baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani
wanapowaona wenzao wameamua kurudi nyumbani CCM kuwa wamenunuliwa au kuahidiwa
vitu fulani, tuwahakikishie wananchi wenzetu kuwa tumeamua kurejea kwa baba na
mama kwa hiari yetu bila kushawishiwa nanyi njooni nyumbani tujenge taifa letu",
alisema Fumpa.
Akihutubia mkutano huo, Bulembo aliwataka wananchi wa
Jimbo la Mbeya mjini kujutia uamuzi wao waliouchukua mwaka 2010 wa kumchaguae
Joseph Mbilinyi 'Sugu'wa CHADEMA kuwa Mbunge wao kwa kutorudia kosa hilo katika
uchaguzi mkuu mwaka 2015.
"Ndugu zangu
kufanya kosa si kosa kosa ni kurudia kosa, mwaka 2010 mlimchagua Sugu wa CHADEMA
kuwa Mbunge wenu, lakini hawasaidii kuleta maendeleo yenu zaidi ya kuipinga
serikali ya CCM kuleta maendeleo, hivyo msirudie kosa hilo katika uchaguzi wa
serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu mwaka 2015", alisema
Bulembo.
Bulembo aliyeko
katika ziara ya kukagua, kuhimiza uhai wa Chama na jumuia zake, kukagua
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mkoani hapa alisema kuchagua upinzani ni
kuthoofisha jitihada za serikali ya CCM ya kuharakisha maendeleo
yao.
Alisema vyama
vya upinzani kikiwemo CHADEMA haitakii mema CCM na vimekuwa vikifanya kila
liwezekanalo kuhakikisha ilani ya CCM inayolenga kuondoa kero na changamoto
zinazowakabili wananchi haitekelezwi, hivyo kuchagua upinzani ni sawa na
kusitisha kwa muda maendeleo yao.CHANZO http://ndgshilatu.blogspot.com/2013/08/chadema-hoi-mbeya-mjini-ccm-yazoa-365.html
No comments:
Post a Comment