Umati
wa watu wakiwemo waliokuwa wateja wa Desi waliofika mahakamani hapo
kujua hatima ya fedha walizopanda wakitoka nje ya mahakama baada ya
kuambiwa hakuna chao.
Wachungaji watano wa makanisa ya Kipentekoste waliokuwa wakishikiliwa
kwa tuhuma kwa kuendesha biashara ya upatu kupitia Taasisi yao ya Desi
Tanzania na kuijipatia fedha kwa njia ya udanganyifu leo mmoja wao,
Albogast Francis ameachiwa huru baada ya kuonekana hana hatia na wengine
wanne wamehukumiwa kwenda kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya
milioni 21 kila mmoja pamoja na kutaifishwa mali zao.Kesi hiyo iliyokuwa ikiunguruma mahakama ya Kisutu Jijini Dar karibu miaka mine iliyopita mahakama hiyo kupitia hakimu wake Aloyce Katemana ilitoa hukumu hiyo baada ya kulidhishwa na ushahidi uliotolewa upande wa utetezi na Jamhuri. Waliopanda Desi nao waambiwa wanakesi ya kujibu.
Picha juu ni baadhi ya matukio yaliyojiri mahakamani hapo...
No comments:
Post a Comment