Rais
Kikwete akiwa na bingwa wa dunia Hamisi Mohamed pamoja na wachezaji
wenzie na viongozi wa timu ya Tanzania iliyoshiriki katika mashindano ya
dunia
Hamisi Mohamed na wenzake wakionesha umahiri wao wa mchezo wa kuruka kamba ambao unazidi kupata umaarufu duniani kote
Hamisi akionesha manjonjo yake Ikulu
Rais Kikwete akiangalia medali kibao alizoshinda Hamisi Mohamed.
Rais
Kikwete akimpongeza kijana Hamisi kwa kutwaa ubingwa wa dunia na
kuipatia sifa Tanzania ambayo kwa miaka mingi haijashinda medali yoyote
katika michezo ya kimataifa.
Mwenyekiti wa Sport Training Centre (TSTF), Dennis Makoi
amesema kuwa walipotambua kuwa kijana
huyo anakipaji cha mchezo huo waliamua kumtafutia mfadhili ili kukiendeleza. Alisema kuwa walipata mfadhili kutoka Marekani ambaye anamiliki
kituo cha kufundishia mchezo huo ambaye alimchukua Hamisi kwenda Marekani
Desemba mwaka jana kwa ajili ya kuendeleza mafunzo hayo.
Makoi alisema kijana huyo akiwa katika kituo cha mfadhili
huyo alishiriki mashindano ya dunia ya mchezo wa kuruka kamba yaliyofanyika
Julai 5 hadi 13 mwaka huu jijini Orlando, Marekani, yaliyokuwa na washiriki 480
kutoka timu 44 kutoka nchi 14 ambapo
jumla ya wachezaji 6 walishiriki kutoka Tanzania na hatimaye kijana huyo
alinyakuwa kombe hilo na kuwa bingwa wa Dunia.
Amy Canady ambaye ni mfadhili wa kijana huyo alisema kuwa
amefurahishwa na jitihada za kijana huyo ambapo anafaa kuigwa na kupewa
usimamizi mkubwa, na kwamba lengo lao ni kujenga kituo cha mchezo huo Tanzania
ili kuukuza ambapo vijana watapata fursa ya kucheza wakiwa nchini
kwao na kuitangaza Tanzania.
No comments:
Post a Comment