WAZIRI
wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amezungumza na waziri
mwenzake wa Syria Walid al-Moualem Alhamisi wiki hii na kumweleza kuwa
serikali yake inapaswa kuruhusu wakaguzi wa silaha wa Umoja wamataifa.
Wakaguzi wa silaha wa Umoja wa Mataifa wanatakiwa kuingia katika maeneo yanayodaiwa kuwa shambulio la gesi ya sumu limefanyika.
Kerry
amepiga simu "kuweka wazi kuwa iwapo, kama inavyodaiwa, serikali ya
Syria haina cha kuficha, inapaswa kuwaruhusu wakaguzi mara moja na
wapewe ruhusa bila ya vipingamizi katika maeneo hayo bad
ala ya kuendelea kuyashambulia maeneo yaliyoathirika na kuzuwia kuingia
kwa wakaguzi pamoja na kuharibu ushahidi" wizara ya mambo ya kigeni
imesema.
Mtu aliyenusurika akijipumzisha baada ya kupatiwa matibabu.
Uhakikisho
"Waziri
Kerry amesisitiza zaidi kwamba amepokea uhakikisho kamili kutoka kwa
makamanda wa jeshi la Syria kuwa watahakikisha kuingia kwa salama
wakaguzi wa umoja wa Mataifa katika maeneo hayo," amesema afisa wa
wizara hiyo.
Kerry
ambaye alishiriki akiwa hayupo katika Ikulu ya Marekani ya White House
katika mkutano kuhusiana na uwezekano wa Marekani kuchukua hatua dhidi
ya kile kinachodaiwa kuwa ni matumizi ya silaha za kemikali nchini
Syria, amefanya mawasiliano kadha na wanadiplomasia kadha jana Jumamosi
na mawaziri wenzake nchini Saudi Arabia, Jordan na Uturuki, afisa huyo
amesema.
Katika
mazungumzo yote hayo kwa njia ya simu , waziri Kerry amesisitiza
umuhimu wa utambuzi wa haraka wa ukweli na kueleza umihumu na athari za
matumizi ya silaha za kemikali, ameongeza afisa huyo.
Waziri John Kerry wa Marekani.
Marekani na Uingereza zajadiliana
Rais
wa Marekani pamoja na waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
wamekaribia jana Jumamosi kuweka lawama za shambulio hilo la gesi ya
sumu karibu na mji mkuu Damascus mikononi mwa majeshi ya rais Bashar
al-Assad.
Taarifa
kutoka ofisi ya waziri mkuu katika mtaa wa Downing imesema kuwa
viongozi wa Marekani na Uingereza , wana wasi wasi mkubwa , kuhusiana na
ishara zinazoongezeka kuwa hilo lilikuwa shambulio la silaha za
kemikali lililofanywa na utawala wa Syria dhidi ya watu wake.
Rais Barack Obam.
"Ukweli
kwamba rais Assad ameshindwa kutoa ushirikiano na Umoja wa Mataifa
kunaashiria kuwa utawala huo una kitu cha kuficha," taarifa hiyo
imeongeza, na kudokeza kuwa " matumizi ya silaha la kemikali
yatasababisha kuchukuliwa hatua kali kutoka jumuiya ya kimataifa."
Serikali
ya Syria pamoja na mahasimu wake wakati huo huo wametupiana lawama kwa
matumizi hayo ya silaha za sumu, wakati shirika la kutoa misaada la
madaktari wasio na mipaka limesema kiasi ya watu 355 wamefariki kutokana
na dalili za "sumu inayoathiri mapafu" kutokana na shambulio la
Jumatano, huku maelfu zaidi wakipatiwa matibabu hospitalini.
Iwapo
itathibitishwa , shambulio hilo litakuwa baya kabisa la matumizi ya
gesi ya sumu tangu Saddam Hussein kutumia gesi ya sumu dhidi ya
wanajeshi wa Iran na maeneo ya waasi wa Kikurdi kaskazini mwa Iraq
katika miaka ya 1980.
Afisa wa Umoja wa Mataifa wa kupunguza silaha Angela Kane.
Huenda mambo yameiva
Mazungumzo
ya Obama na washauri wake wa masuala ya usalama yamekuja siku moja
baada ya waziri wa ulinzi Chuck Hagel kusema wizara yake imewasilisha
mapendekezo kadha kwa rais na ameeleza kuwa majeshi ya Marekani
yanasogezwa karibu kwa uwezekano wowote wa uamuzi wa kuchukua hatua
dhidi ya utawala wa Syria.
Wakati
huo huo mkuu wa idara ya kupunguza silaha duniani wa Umoja wa Mataifa ,
Angela Kane, amewasili mjini Damascus siku ya Jumamosi ( 24.08.2013)
kutoa msukumo kwa serikali ya Syria kuwaruhusu wataalamu wa Umoja huo
kuchunguza madai ya matumizi ya silaha za sumu. DW
No comments:
Post a Comment