Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, August 16, 2013

KONDA WA DALADALA IRINGA AONJA JOTO YA JIWE,AFAANYISHWA USAFI WA DAMPO BAADA YA KUKAMATWA AKIJISAIDIA HAJA NDOGO HADHARI.


 Kijana  anayefanya kazi ya  ukonda katika daladala  inayofanya safari  zake kati ya  Kitapilimwa - M.R miyomboni  Bw  Christipher Kinigo akifanya  usafi  wa  kuzoa  taka kwa  mikono baada ya  kunaswa  akijisaidia haja ndogo  katika  eneo hilo kinyume na sheria  za usafi  Manispaa ya  Iringa
 Hapa  akitafakari  jinsi ya  kuzoa  taka kwa  mikono baada ya kushindwa  kulipa faini ya Tsh 50,000 iliyopangwa na Manispaa ya  Iringa kwa  wachafuzi wa mazingira
 Hapa  akiwajibika  kufanya  usafi
 Hapa  koda  huyo Bw  Christopher  anayefanyia kazi katika  daladala  lenye namba T 228 AMV akizoa  taka katika  dampo la M.R  mchana  wa  leo
Konda  huyo akiwa katika  daladala analofanyia kazi baada ya  kufanya  usafi kama adhabu ya  kuchafua mazingira.
KONDA  wa daladala lenye namba T 228 AMV inayofanya safari  zake kati ya Kitapilimwa na M.R- Miyomboni mjini Iringa Bw  Christopher Kinigo amepewa adhabu ya  kuzoa  taka katika  dampo  kwa mikono baada ya kukutwa akijisaidia haja ndogo kituo cha daladala M.R kando ya  barabara ya Mkwawa .

Kijana  huyo amekamatwa  leo  na  wadau  wa mazingira  mjini Iringa ambao  wamekuwa  wakifanya kazi na mtandao  wa matukio  daima katika  kuweka mji  wa Iringa na mkoa wa Iringa katika hali ya  usafi.

Hatua  ya  kijana  huyo  kufanyishwa  usafi  imekuja  baada ya kuangua  kilio akiomba  kusamehewa  kutokana na kosa  hilo na kuwa  hakuwa na  fedha kiasi  cha  Tsh 50,000 ambazo ni faini za  kisheria   kwa  wanaokamatwa kwa  kuchafua mazingira katika mji  wa Iringa.

Akizungumza  baada ya  kutekeleza  zoezi hilo la usafi  kijana  huyo alisema  kuwa ugeni  ndio ambao unamsumbua na  kuwa anatambua  kosa lake na  kuwataka  vijana  wenzake na  wananchi  wengine  kuepuka  kuchafua mazingira katika mji  wa Iringa.

Kwa mujibu  wa mwanasheria  wa Manispaa ya  Iringa Innocent Kihanga  mwananchi atakayekutwa anachafua  mazingira kwa  kutupa  taka ovyo ama  kujisaidia maeneo yasiyo  rasmi faini yake Tsh 50,000  na mkamataji atalipwa  Tsh 20,000 na  fedha  nyingine  zitaingizwa katika mfuko  wa usafi  wa mazingira mjini Iringa.

Hivyo  kuwataka  wananchi  kuendelea  kuwakamata  na kuwafikisha  ofisi ya manispaa ya  Iringa  wale  wote wanaochafua mazingira  ovyo .

Huku  mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa Terresia Mahongo  akipongeza jitihada za  wadau  wa mazingira mjini  Iringa na kutaka kila mwananchi  kuhakikisha  eneo lake  ni safi .

No comments:

Post a Comment