Madam Rita |
wa kumfungulia mashitaka kwa kuwa hatakuwa na pesa za kumlipa kwa maana itakuwa kesi ya kumchafua na inaweza kumgharimu pesa nyingi.
.
Madam Rita ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha burudani cha The Strengo Saturday kinachorushwa na Radio Victoria fm kupitia 90.6 kilichopo Musoma, Mara. Ambapo mtangazaji wa kipindi hicho Patrick Derrick Mwankale alitaka kujua sababu kubwa ya EBSS kuhamishiwa katika kituo cha televisheni cha TBC1 ikitokea ITV na vipi kuhusiana na habari zilizopo za yeye (Madam Rita) kutaka kumfungulia Nay Wa Mitego kesi ya kumchafua . " unajua patrick nashangazwa sana na hizi taarifa zilizopo katika mitandao ya kijamii pamoja na vyombo vya habari, mimi sina mpango wa kumfungulia kesi mahakamani maana mimi ninajua anatafuta kick kupitia jina langu , anatafuta kuendelea kukaa katika soko la muziki kupitia jina langu, nikimfungulia kesi ya kunichafua mimi hatakuwa na hela ya kunilipa kabisa na kwanza nitakuwa napoteza muda wangu wa kusumbuana naye nakuzidi kumuweka juu zaidi. unajua mimi kwanza hata simfahamu, sijawahi kukutana naye, sijawahi hata kukaa nae na hapo ndipo nitalazimika kumtafuta ili nimjue, lakini kuhusu kumfungulia kesi siwazi kabisa maana hana hela ya kunilipa huyo" alisema Madam Rita
Madam Rita akionekana kuumizwa zaidi na taarifa hizo, amesema , huyo msanii ni kati ya wasanii wasiojitambua kabisa wala kujielewi. Maana kabla ya kuimba chochote anatakiwa kufanya reasech ya kutosha na siyo kuropoka ujinga kujitafutia kick , kwa kuwa hata watanzania pamoja na wasanii wenyewe wanamshangaa kwa hayo anayosema na kuimba. Kila mtu anajua kuwa hela na zawadi zinazotangazwa zinatoka na siyo propaganda na kama ni swala la msanii kutokusikika au kuvuma baada ya yeye kutolewa na shindano hilo hiyo ni juu yake binafsi.
Pia alisema hakuna sababu kubwa sana iliyopelekea EBSS ya mwaka huu kuhamishiwa TBC1 zaidi ya maslahi ya kibiashaa .Na pia ndio channel ambayo hivi sasa ina watazamaji wengi kutokana na ishu ya ving'amuzi kwasababu ITV kuna baadhi ya mikoa haikamati kwa sababu ya ishu hiyo ya ving'amuzi
No comments:
Post a Comment