Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 1, 2013

MAMA SALMA AHUDHURIA NA KUFUNGA RASMI MKUTANO WA HIGH LEVEL GROUP HUKO BOTSWANA.

IMG_8866 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa rasmi kwenye mkutano wa “High Level Group” na Dr. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS Regional Support Team kwa  nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika  katika siku ya pili ya  mkutano huo unaofanyika jijini Gaberone nchini Botswana tarehe 31.7.2013.PICHA NA JOHN LUKUWI WA MAELEZO IMG_8900Baadhi ya wajumbe wa mkutano wakisoma jarida linalochapishwa na Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, huku wakiendelea na mkutano. IMG_8909Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akifunga rasmi mkutano wa High Level Group uliokuwa unafanyika kwenye hoteli ya Lasmore nchini Botswana tarehe 31.7.2013. IMG_8922Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akifunga rasmi mkutano wa High Level Group uliokuwa unafanyika kwenye hoteli ya Lasmore nchini Botswana tarehe 31.7.2013. IMG_8941Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Profesa Alaphia Wright, Mwakilishi wa UNESCO kwenye nchi za ukanda wa Kusini mwa Afrika mwishoni mwa mkutano wa siku mbli wa High Level Group ulikuwa ukifanyika jijini Gaberone nchini Botswana tarehe 31.7.2013.IMG_8954Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsikiliza kwa makini Dr. Patricia Machawira, Mshauri wa HIV na AIDS kwa nchi za ukanda wa Mashariki na Kusini mwa Afrika mwishoni mwa mkutano wa siku mbili uliokuwa unafanyika nchini Botswana. Dr. Machawira alikuwa akimshukuru Mama Salma kwa ushiriki wake kwenye mkutano huo uliofanyika tarehe 30.7 hadi 31.7.3013. IMG_9048Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihojiwa na na MS Sandra Chuma kutoka kwenye sekretarieti ya High Level Group, kuhusu masuala mbalimbali yanayowakabili wanafunzi yanayohusiana na elimu na afya, mwishoni mwa mkutano. IMG_9069Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiagwa rasmi na Mwakilishi wa UNESCO wa Kanda ya Kusini mwa Afrika Profesa Alaphia Wright nje ya hoteli ya Lasmore huko Gaberone nchini Botswana ulikofanyika mkutano wa siku mbili wa High Level Group kwa nchi za  Mashariki na Kusini mwa Afrika kuhusiana na elimu na afya kwa vijana.

No comments:

Post a Comment