skip to main |
skip to sidebar
MAMNOON RAIS MPYA PAKISTAN
Wabunge wa Pakistan wamemchagua Mamnoon Hussain, mgombea wa chama tawala, kama rais mpya wa nchi hiyo. Uchaguzi wa wadhifa huo ambao hauna mamlaka mengi, hata hivyo ulisusiwa na kundi kuu la upinzani.
Tume ya uchaguzi imesema Hussain, aliyeteuliwa na chama cha Waziri Mkuu Nawaz Sharrif cha Pakistan Muslim League, amepata kura 432.
Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 73 kutoka mji wa kusini wa bandari Karachi, ni veterani mtiifu wa chama tawala. Wajihuddin Ahmed, jaji wa zamani wa mahakama ya juu na mgombea wa chama cha nyota wa mchezo wa kriketi Imran Khan cha Movement for Justice, alipata kura 77. Hussain atachukua nafasi ya rais anayeondoka Asif Ali Zardari, ambaye muhula wake wa miaka mitano unakamilika mwezi Septemba.
No comments:
Post a Comment