Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 10, 2013

Man united yachapwa 3-1 na sevilla

 man u2 90302
Marin akifunga (HM)
man u d290b
MAMBO yameendelea kuwa magumu katika hatua za mwanzoni kwa kocha David Moyes, baada ya leo Manchester United kuchapwa mabao 3-1 na Sevilla katika mechi maalumu ya kumuaga Rio Ferdinand Uwanja wa Trafford.

Katika mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki zaidi ya 40,000, mabao ya Sevilla yamefungwa na Perotti dakika ya 21, Marin dakika ya 25 na Rabello dakika ya 91, wakati bao la kufutia machozi la United limefungwa na Valencia dakika ya 65.
 
Kikosi cha Manchester United kilikuwa; De Gea, Fabio, Ferdinand, Smalling, Buttner, Valencia/Carrick dk65, Anderson/Giggs dk65, Cleverley/Jones dk46, Januzaj, Kagawa/Zaha dk65 na Henriquez/Lingard dk46.
 
Sevilla: Beto, Figueiras, Fazio, Pareja/Puerto dk56, Alberto, Medel, Kondognbia, Marin, Perotti, Vitolo na Bacca. Chanzo: sportmail

No comments:

Post a Comment