JIJI
LA MBEYA LAJIPANGA KUHAKIKISHA USAFI WA MAZINGIRA UNAIMARISHWA.
ATAKAYEKAMATWA
KUTUPA UCHAFU OVYO KULIPA FAINI 50,000/=.
ATAKAYEMKAMATA
NA KUMPELEKA MTUPA TAKA OVYO ATAPEWA 20,000/= PAPO HAPO.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amelazimika
kuingilia kati kunusuru hali ya uchafu iliyokithiri ndani ya jiji la Mbeya kwa
kuwataka Viongozi kusimamia Sheria.
Kandoro amesema Jiji la Mbeya ndiyo taswira ya
Mkoa mzima hivyo hali ya uchafu inapozidi inatoa picha ya Mkoa mzima ambao
utaonekana kuwa na sifa ya uchafu.
Amesema Jiji la Mwanza linaloongoza kwa Usafi kila
Mwaka lina watu na wananchi kama wanaoishi Mkoani Mbeya husasani katikati ya
Jiji la Mbeya na kushangazwa na kitendo cha kutopenda hali ya usafi.
Kutokana na hali hiyo Kandoro ameagiza viongozi
wa Serikali za Mitaa, Kata na Halmashauri ya Jiji kuhakikisha wanasimamia na
kutekeleza sheria ya Usafi wa mazingira na matokeo yake yapatikane ndani ya
mwezi mmoja.
Hivyo sheria ya Halmashauri ya Jiji la Mbeya
inasema atakayebainika kutupa takataka sehemu isiyoruhusiwa atalipa faini ya
Shilingi 50,000/= huku mtu yeyote atakayemkamata anayetupa taka na kumfikisha
kunakotakiwa atalipwa 20,000 papo hapo.
Hayo yamebainishwa katika mkutano wa Wadau wa
Usafi wa Mazingira ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro
uliofanyika katika ukumbi wa Mkapa Sokomatola Jijini Mbeya.
Kutokana na maagizo hayo baadhi ya wajumbe
waliohudhuria mkutano huo wameunga mkono suala hilo na kwamba ajira
zitaongezeka kwa vijana kuwawinda wanaochafua mazingira na kujiongezea kipato.
Na mbeya yetu
|
No comments:
Post a Comment