Chande Abdallah na Mayasa Mariwata
MSAKO mkali unaendelea kuvifumua vibanda vya video vinavyokiuka maadili kwa kuonesha mikanda ya ngono ‘X’ kwa watoto.
Tukio la hivi karibuni limetokea Tandale Uzuri jijini Dar ambapo
vijana wawili, Yasini Issa (25) na Kivuluga Abdi (27) wametiwa mbaroni
kutokana na kudaiwa kuendesha biashara hiyo haramu.
Kabla ya tukio
hilo, baadhi ya wazazi wanaoishi eneo hilo walipiga simu katika ofisi za
gazeti hili wakilalamikia matukio hayo ya watoto kuoneshwa mikanda hiyo
inayokiuka maadili ya Kitanzania.
Baada ya kupata ukweli wa tukio hilo, Jumatatu iliyopita waandishi
wetu kwa kutumia kitengo cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM),
waliwasiliana na Polisi wa Kituo cha Magomeni na kujipanga kufanikisha
zoezi la kuwatia mbaroni wahusika.
Upelelezi wa OFM uligundua kuwa
kibanda hicho kilikuwa kikianza kuonesha mikanda hiyo michafu kuanzia
saa mbili za usiku na kuendelea.
Mmoja wa wandishi wetu alijifanya mteja wa kuangalia sinema katika
kibanda hicho na kulazimika kuingia katika kibanda hicho kwa kulipa
shilingi 400.
Akiwa ndani ya kibanda hicho, aligundua kuwepo kwa watu
wa jinsi tofauti na watoto wakiendelea kuangalia sinema mbalimbali
zilizokuwa zikioneshwa.
Mwandishi huyo alikuwa akiwasiliana na mwenzake aliyekuwa nje ya kibanda cha video pamoja na askari wa Kituo cha Magomeni.
Ilipotimu
saa mbili kamili, picha zilizokuwa zikioneshwa ndani ya kibanda hicho
zilibadilishwa na kuwekwa CD za X huku watoto wakiwa wamejaa ndani.
Mwandishi wetu aliwafahamisha askari kwamba mchezo ulikuwa umeshaanza
nao wakafika na kukuta tukio hilo likiendelea huku watu waliojazana
ndani ya kibanda hicho wakikimbia na kuwaacha wahusika waliotiwa
nguvuni.
Baada ya askari kufanya ukaguzi ndani ya jengo hilo
walizikuta kondomu zilizokuwa zimeshatumika ambazo inadaiwa baada ya
watu kuangalia picha hizo walikuwa na tabia za kufanya ngono ndani ya
kibanda hicho.
Mwisho, watuhumiwa walibebeshwa vitendea kazi vyao na kupelekwa
katika Kituo cha Polisi Magomeni na kufunguliwa kesi ya KUONESHA PICHA
ZA NGONO yenye kumbukumbu namba MAG/RB/9722/2013.
MAHAFALI YA 16 KIDATO CHA NNE KOM SEKONDARY YAFANYIKA
-
Wahitimu wa mahafali ya 16 kidato cha nne mwaka 2024 shule ya Sekondari Kom
wakipokea keki kwa niaba ya wahitimu wengine.
Wahitimu wa kidato cha nne 2024 s...
11 hours ago
No comments:
Post a Comment