Isitoshe, kulikuwa na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama machinga ambao kwa kawaida hupanga biashara zao kwa utaratibu na sasa wamebanwa kwenye viambaza vya kuta za majengo kupisha magari kupaki kuzunguka soko.
Mstahiki Meya Jerry Silaa tunaamini ni msomi na umetembea kwenye miji ya wenzetu. Kinachofanyika Kariakoo nahofia hukijui, lakini, ni uhuni. Halmashauri inaweza kubuni miradi mingine ya kukusanya mapato, lakini hili la kumpa mtu tenda ya kuweka parking kuzunguka soko la Kariakoo ni kero itakayopunguza watembeleaji wa soko na hivyo mapato pia.
Sisi kama watembeleaji wa soko hilo tunakuomba Mstahiki Meya, Jerry Silaa uliweke hili mezani kwa Waheshimiwa Madiwani wenzako na mlifanyie kazi.
Maggid. ( Mkazi wa zamani wa Ilala).CHANZO MJ
No comments:
Post a Comment