Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 22, 2013

Mwanamuziki nguli Maalim Gurumo astaafu rasmi shughuli za muziki.


GURUMO
Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo (katikati) akizungumzia kustaafu rasmi kazi ya muziki aliyoifanya kwa muda wa miaka 53 katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam leo. (Picha na Magreth Kinabo).
Mwanamuziki mkongwe wa bendi ya Msondo Ngoma Mzee Muhidin Gurumo amestaafu rasimi kazi ya muzika alioifanya kwa muda wa miaka 53.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mzee  Gurumo mwenye umri wa miaka 73 amesema ameamua kustaafu kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe kutokana na umri wake kuwa mkubwa.
Mzee Gurumo amesema “Muziki kwangu umekuwa kama asili yangu na kazi yangu lakini nimeamua kustaafu kutokana na umri wangu na nitabaki kuwa mshauri tu kwa mwanamuziki yeyote atakayetaka ushauri wangu” .
Pamoja na kufanya kazi ya muziki Gurumo amesema kuwa hakupata mafanikio makubwa zaidi ya kujenga nyumba anayoishi na familia yake.
 Amesema ameimba kwa muda mrefu sana lakini hata baiskeli hana, hata hivyo Mzee Gurumo akasema anashukuru kuwa ana nyumba ya kuishi na familia.
 Vilevile Mzee Gurumo amewaasa vijana kuwa wabunifu na kuupenda mziki wa zamani, kwani ndio chimbuko la bongo fleva na kuwashauri wanamuziki wa sasa kuwa wavumilivu kukaa muda mrefu kwenye bendi moja ili hata wanapoondoka mchango wao uthaminiwe.
 Mzee Gurumo  ambaye ana mke na watoto wanne amesema kuwa katika maisha yake ya muziki alifanikiwa kutunga nyimbo 60,000 na anavutiwa zaidi na mwanamziki Hussein Jumbe na Hassani Rehan Bichuka na kwa wanamuziki wa kizazi kipya anavutiwa na Nassibu Abdul ’Diamond’.
Mwanamuziki huyo mkongwe alianza kufahamika katika tasnia ya muziki wa dansi kwenye miaka ya 1960, ambapo mwaka 1964 alikuwa miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Mlimani Park.
Alidumu na Mlimani Park mpaka mwaka 1985 na kuhamia Safari Sound, aliyofanya nayo kazi mpaka mwaka 1990 na kujiunga na Msondo Ngoma mpaka sasa anaamua kustaafu Muziki.

No comments:

Post a Comment