Mamia ya
raia wameuawa kufuatia shambulio lililotumia silaha za kemikali viungani
mwa Mji Mkuu wa Syria, Damascus. Makundi ya upinzani yanasema makombora
yaliyokua na kemikali ya sumu yalilenga eneo la Ghouta usiku wa kuamia
Jumatano.
Inadaiwa
majeshi ya serikali yalikua yakiwashambulia waasi.Hata hivyo Shirika la
utangazaji la serikali limetaja taarifa hizo kama upuzi mtupu,na kusema
ni kisingizio tu cha kuwachochea wakaguzi wa Umoja wa Mataifa walioko
Syria.
Muungano wa
upinzani umesema zaidi ya watu 650 waliuawa katika shambulizi
hilo.Makundi mengine ya kiraia pia yametangaza vifo vya mamia katika
shambulio hilo japo taarifa hizo hazijathibitishwa kirasmi.
Waziri wa
mambo ya nje wa Uingereza William Hague, ametaka utawala wa Syria
kukubalia wakaguzi wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo na kusema
Uingereza itawasilisha hoja katika Umoja wa Mataifa.
Muungano
wa nchi za Kiarabu pia umeunga mkono wakaguzi hao kuingia eneo
hilo.Shambulizi hilo ni moja wapo ya operesheni kali ya jeshi la
serikali katika maeneo yanayothibitiwa na waasi mjini Damascus.
Maeneo yaliyoathirika na shambulio la karibuni ni pamoja na Irbin,Duma na Muadhamiya.
No comments:
Post a Comment