alikuwa ni mmoja wa wasemaji, watoa maada mbele ya mamia ya wakazi wa Tabora katika kuhamasisha vijana kuzijua fursa na kuzitumia ili kujiletea maendeleo katika maisha yao. Kwa mujibu wa Diamond, mwaka 2008 na 2009 alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha mabegi kilichoko Mikocheni na kulipwa mashahara wa shilingi 2,000 kwa masaa 8, huku nauli ikimgharimu shilingi 1,000 mpaka kufika kwao na hapo chakula ni zaidi ya shilingi 1,000.
“Ukimuona mtu ana mafanikio kiukweli ujue amehangaika sana, mimi katika maisha yangu sikuwahi kufikiria kama ningelikuja kupanda ndege kwa kutumia pesa yangu, namshukuru sana Mungu na haya ni matunda ya kazi ngumu ambazo huwa nazifanya,” alisema. Msanii huyo aliwataka wapenzi wa kazi zake kufanya kazi kwa bidii kwa kipindi kifupi ili kufanikiwa katika maisha yao na kuonekana watu katika jamii na sio kudharaulika.
No comments:
Post a Comment