Wasanii
maarufu wa kizazi kipya zaidi ya Kumi tano watatoa burudani kwa mara ya
kwanza kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara na majirani zake katika tamasha
kubwa la Serengeti Fiesta 2013 ambalo ni maarufu kwa ”Tupo Pamoja,
Twenzetu, Tukawinde” Ni Noma sanaa” litalofanyika katika uwanja wa
Nangwanda Sijaona uliopo mjini Mtwara. Burudani hiyo itakuwa kivutio
tosha kwa wakazi wengi kutokana na kundi kubwa la wanamuziki wa kizazi
kipya waliopo kwenye chati za juu katika muziki huo.
Tamasha hilo linaambatana na shamrashamra zinazoendelea kwenye
promosheni za bar mjini hapo ambapo wakazi wa Mtwara watakuwa
wakijishindia tiketi za bure pamoja na fulana baada ya kujibu maswali
marahisi, pia kutakuwa na washindi ambao watapata nafasi ya kuwakilisha
Mtwara kwenye tamasha la kuhitimisha msimu wa Fiesta 2013 jijini Dar Es
Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari Meneja wa bia ya Serengeti Premium Lager ambayo
ndio bia inayodhamini tamasha hili kubwa, Allan Chonjo alisema ”Mpaka
sasa tumepata wawakilishi kumi na moja Lydia Bitwale, Belinda Mgongorwa,
Samweli Aloyce, Josiah Naftael na Severine Matata kutoka Kigoma, Issa
Jaffary, Jayson Baduga na Augistino Massawe Kutoka Tabora na Singida ni
Richard Mmassy, Emmanuel Nagunwa na Rose Tarimo”.
”Washindi wote kutika mikoani watakaa jukwaa la watu maalumu ambapo wataweza kushuhudia burudani kwa karibu zaidi na watapata nafasi ya kupiga picha na wasanii wakubwa, hivyo tunawaomba wakazi wa
Mtwara waendelee kunywa bia ya Serengeti ili waweze kujishindia bia za bure na hatimaye kushinda nafasi hiyo ya kuja Dar Es Salaam kwa ajili ya Fiesta ya mwisho”. Wateja wanatakiwa kuangalia chini ya kizibo na kuona kama wajishindia bia za bure kwani kuna bia zaidi ya laki mbilli nchi nzima, aliongeza Chonjo.
Msanii mkali katika miondoko ya kipwani Snura, ambaye ni maarufu kwa wimbo wake wa ”majangaa” ataungana na wasanii wengine waliofanya vizuri kwenye tamasha hilo lililoanzia mkoani Kigoma ambapo ilikuwa kwa mara ya kwanza pia, ikafuatiwa na Tabora na Singida wikiendi iliyopita. Wasanii zaidi ya kumi na tano wanaokubalika kama Nay wa Mitego, Makomandoo, Juma Nature, Matonya, Kassim Mganga, Chege na Temba, Snura, Madee, Young Killer, Stamina, Godzilla, Nikki Wa Pili, Ommy Dimpoz, Kalapina na Pasha ambaye anatokea mkoani Mtwara watapanda jukwaani kukonga nyoyo za wakazi wa mji wa Mtwara siku ya Jumamosi
No comments:
Post a Comment