Mahmoud Ahmad Arusha
Mamlaka ya mapato
Tanzania(TRA)imetoa elimu ya mlipa kodi kwa wasanii wa filamu na mziki
wa mkoa wa Arusha ilikuweza kudhibiti wizi wa mapato yatokanayo na kazi
za wasanii hapa nchini.
Akizungumza na vyombo vya
habaribaada ya kuwezesha kutoa mafunzo kwa wasanii wa mkoa wa Arusha
afisa mwandamizi huduma kwa walipakodi makao makuu Msafiri Mbibo amesema
kuwa wapo katika mchakato wa kuhakikisha uchumi unakuwa kwa kuchukuwa
hatua mbali mbali za kuhakikisha wanaziba mianya iliyokuwa ikilikoseha
taifa mapato.
Mbibo alisema kuwa wizi wa kazi
za wasanii imekuwa ndio njia ya kulikosesha taifa mapato na kuwaacha
wenye haki miliki wakiendelea kufa maskini huku wauzaji wakinufaika na
jasho la wanyonge.
Akawataka wasanii kuchukuwa
hatua za kuweza kudhibiti kazi zao kwa kuziweka stamp za mamlaka hiyo
kwani stamp hizo zinauzwa kwa tsh 44 tu kwa cd pamoja na box lake
mkizembea mtakuwa mmetoa mianya kwa watu mbali mbali kujinufaisha kwa
njia isiyo halali kutokana na kazi zenu.
“unajua Tanzania inaendelea
kuchukuwa hatua mbali mbali za kuinua uchumi wake na katika njia hizo
hii ni mojawapo inayolikosesha taifa mapato na kuwanufaisha watu
wachache tena wezi wa haki miliki za kazi za wasanii”alisema Mbibo.
Imeonekana kuwa wizi wa kazi za
wasanii kwa njia ya kughushi na kusambaza ni moja ya changamoto
zinazowakabili wadau wa tasnia hiyo ikiwemo utengenezaji wa mikataba ya
kinyonyaji inayowafanywa na watu wenye nguvu ya kiuchumi kwa wasanii
hapa nchini hivyo kukosa mapato stahiki ya kazi zao.
Kazi za wasanii hawa zimekuwa
zikiburudisha kuelimisha na vile vile zimekuwa zikichangia kwa ujumla
uchumi wa taifa letu kwa njia ya kuuza nje na hapa ndani ya nchi bidhaa
hizo na kuinua uchumi endelevu kwa baadhi ya wasanii wengi wao
kuendelea kunyonywa kazi zao.
Kuanzia sasa wauzaji na
watengenezaji watalazimika kulipia kodi kwa kuweka stamp katika cd
zitokazo nje na ndani ya nchi ilikuweza kuokoa fedha zinazopotea
kutokana na kudurufu kazi za wasanii hapa nchi na wa nje ya nchi.
Huku serekali ikiendelea
kuchukuwa hatua mbali mbali katika kuboresha na kuinua uchumi kwa kutoa
mafunzo kwa wadau mbali mbali hatua zinazofikiwa kati kufikia uundaji wa
mfumo husika utakaodhibiti mapato ya kazi za wasani hapa nchini
iliwaweze kunufaika na kazi zao.
Kazi zao baada ya kusajiliwa
kwenye mamlaka husika ikiwema COSOTA NA BASATAhuku wasanii wa filamu
wakijisajili Bodi ya filamu Tanzania na Cosota na baada kupatiwa stamp
za TRA
No comments:
Post a Comment