Jeshi
la polisi mkoani Morogoro kwa kushirikiana na maafisa wa hifadhi ya
taifa ya wanyamapori Tanzania TANAPA kutoka hifadhi ya milima ya
udzungwa linawashikilia VIJANA wawili kutokana na tuhuma za
kupatikana na vipande vya meno ya tembo vyenye Thamani ya zaidi
shilingi milioni 39.
Meno
hayo yenye uzito wa kg 45.5 yamekamatwa na jeshi la polisi katika
eneo la mikumi yakiwa yamepakiwa kwenye gari aina ya MISTUBISH FUSO
yenye namba T199 AQP ambayo yalikuwa yamechanganywa kwenye mzigo wa
magunia ya mchele katika harakati za safirishwa kutoka Ifakara
kuelekea jijini Dar es salaam.
Kamanda wa
polisi mkoa wa Morogoro Bw Faustine Shilogile amesema watuhumiwa hao
ambao majina yao yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi walikamatwa na
vipande hivyo usiku wa agosti kumi na tano eneo la Zombo wilayani
Kilosa wakati wakiwa wamepakia vipande hivyo katika harakati za
kuvisafirisha kuelekea jijini Dar-es-salaam.
Kwa
upande wake mkuu wa hifadhi ya Taifa ya Udzungwa Bwana Nitalis uruka
amesema kumekuwepo namatukio ya mara kwa mara ya kukamatwa kwa meno ya
tembo katika hifadhi hiyo hivyo kunahitajika jitihada za makusudi kwa
kuwashirikisha wananchi ili kudhibiti hali yo.
Naye
mkuu wa kikosi cha kuzuia ujangiri kanda ya mashariki inayohusisha
mikoa ya Morogoro Pwani Dar e s salaam na Lindi idara ya wanyama
pori na wizara ya maliasili na utalii bwana Faustine Masalu
amewasisitiza wananchi kukabikiana na vitendo hivyo ili kuhifadhi
rasilimali kwa maslahi ya vizazi vijavyo .
Jamii
imesititizwa kushirikiana na jeshi hilo pamoja na maafisa wa hifadhi za
wanyamapori kuwafichua watu wanaojihusisha na vitendo vya ujangili ili
kukabiliana na changamoto hiyo ambayo inahatarisha usalama wa rasilimali
za nchi.Chanzo Climate Change
No comments:
Post a Comment