Polisi
24 wa Misri wameuawa huko Sinaii katika shambulio lilotokea leo
asubuhi. Wakati huo huo Wizara ya mambo ya ndani nchini Misri imetowa
taarifa za kuuawa kwa Wafuasi 36 wa chama cha Muslim Bradherhood ambao
walikuwa wametiwa nguvuni wameuawa jana kwa bomu za kutowa machozi
wakati waloipojaribu kutoroka pindi polisi ilipokuwa ikiwahamisha katika
jela nyingine karibu na jiji la Cairo.Wizara
hiyo ya mambo ya ndani nchini Misri imesema watu 36, ni wafuasi wa
chama cha rais wa zamani aliepinduliwa na jeshi na kukamatwa Julay 3,
ambapo vyombo vya usalam nchini humo vimesbabisha umwagaji wa damu
mkubwa wakati wa kuwasambaratisha waandamanaji wanaoendelea kudai
kurejeshwa madarakani mwa rais Mohamed Morsi.
Watu
mia nane wamepoteza maisha nchibni Misri kwa kipindi cha siku tano,
huku kiongozi wa kijeshi nchini humo akiapa kuendeleza mapambano dhidi
ya waandamanaji.
Hayo
yanajiri wakati wawakilishi wa nchi 28 za Umoja wa Ulaya wakitaraji
kukutana leo jijini Bruxels kujadili kuhusu hali inayoendelea nchini
Misri.
Kiongozi
wa kijeshi jenerali Abdel Fattah al-Sissi ambaye amezungumza jana kwa
mara ya kwanza tangu kutokea mauaji ya watu mia sita jumatano juma
lililopita amesema kuwa jeshi halitovumilia hali yoyote ile ya vurugu na
lipo tayari kupambana kwa kutumia nguvu kubwa ili kukomesha maandamano,
bila hata hivo kujali kauli za viongozi wa magharibi wanaosema kuwa
kunafanyika umwagaji wa damu.
Abdel Fattah al-Sissi |
Jijini
Bruxels mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Umoja
wa Ulaya unafanyika, ikiw ani kikao cha kwanxza cha kidiplomasia cha
hali ya juu kufanyika juu ya kuzungumzia hali ya nchini misri.
Jana
Jumapili viongozi wa Umoja wa Ulaya, Herman Van Rompuy na jose Manuel
Barroso wametahadharisha seriakli ya Misri kwamba Umoja wa Ulaya upo
tayari kutathimini upya uhusiano wake na Misri iwapo haitositisha
uwamgaji wa damu ambapo jukumu la kurejesha utulivu ni la jeshi na
serikali.
Serikali
nchini humo imewazikataza kamati za umma, zinazoundwa na makundi ya
vijana wanaomiliki silaha ambao wamekuwa wakiwashambulia wale wote
wanaoonekana kuwa ni wafuasi wa Muslim Bradherhood wanaofuga ndevu na
wanawake wanaojisitiri kwa hijabu, pamoja pia na waandishi wa habari wa
kigeni wanaotuhumiwa kumuunga mkono rais aliepinduliw amadarakani
Mohamed Morsi. Baada ya kuwaacha vijana hao wakiendesha machafuko,
hatimaye serikali hiyo hiyo imewatuhumu vijana hao kuendesha vitendo
vilivyo kinyume cha sheria.
No comments:
Post a Comment