RPC MICHAEL KAMUHANDA (ALIYEHAMISHWA)
KLABU ya waandishi wa habari mkoa wa
Iringa (IPC) imetangaza rasmi kumaliza mgogoro na jeshi la polisi baada
ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda
kuondolewa mkoani hapo na nafasi yake kuchukuliowa na kamanda mpya
Ramadhan Mungi.P.T
Mwenyekiti wa IPC Frank Leonard ametoa tamko hilo la kumaliza mgogoro na jeshi la polisi mkoa wa Iringa ,leo katika mkutano mkuu maalum wa UTPC uliomalizika leo katika ukumbi wa Hotel ya Gorden Hotel mjini Dodoma.
RPC MPYA IRINGA BW.RAMADHAN MUNGI
Bw Leonard alisema kuwa hatua ya IPC
kutoa tamko hilo ilikuja baada ya Kamuhanda kuhusishwa na kifo cha Daudi
Mwangosi aliyekuwa mwenyekiti wa IPC ." Ndungu wajumbe wa UTPC napenda kuwatangazia sasa kuwa mgogoro wetu na jeshi la polisi Iringa umemalizika baada ya RPC Kamuhanda kuhamishwa mkoani Iringa na sasa tunaendelea kufanya kazi na jeshi la polisi Iringa"
Siku ambayo aliyekuwa mwenyekiti wa IPC marehemu Daudi Mwangosi alipouwawa katika kijiji cha Nyororo wilaya ya Mjufindi ilikuwa ni septemba 2 /2012 siku ya jumapili majira ya saa 10 jioni.
Na Francis Godwin
No comments:
Post a Comment