Mapigano
hayo yamekuja kufutia ugomvi uliozuka kutokana na kugombania maeneo ya
malisho ambapo wakielezea tukio hilo wafugaji wa jamii ya wabarbai
wamesema chanzo ni mkulima mmoja kuuza shamba la malisho kwa wafugaji
wawili hali iliyozua kutokuelewana baada ya wafugaji kujikuta wakilisha
mifugo katika shamba moja ndipo ulipozuka ugomvi na mapigano na
kuuwawamfugaji mmoja jamii ya Mbarbai na baadaye wakalipiza kisasa kwa
kuumua mfugaji wa kimasai.
Kufutia
mapigano hayo serikali ya wilaya na Kamati ya Ulinzi na Usalama
walilazimika kufanya mikutano kwa makundi hayo ya wafugaji ambapo mkuu
wa Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka amesema serikali itawakamata
waliohusika na mauaji ya wafugaji hao huku akiwataka wafugaji wavamizi
wa mashamba kuondoka ndani ya siku saba katika maeneo hayo ambayo si
rasmi kwa shughuli za ufugaji.
Katika
tukio jingine watu wasiofahamika wamemuuwa kikatili mfugaji mmoja
jamii ya wamasai mkazi wa kijiji cha Twatwatwa wilaya ya Kilosa na
kuzikwa nusu katika mashamba ya mkonge ambapo wananchi wameomba
serikali kutafuta waliohusika na tukio hilo huku kamanda wa polisi Mkoa
wa Morogoro Faustine Shilogile amesema uchunguzi unaendelea na baadhi ya
watu wanashikiliwa kuhusika na mauaji hayo.
No comments:
Post a Comment