Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, August 4, 2013

WAZIRI WA ZAMANI CYPRUS AHUKUMIWA JELA MIAKA 5


/Defense-Minister-Costas-Papacostas.jpgWaziri wa zamani wa ulinzi nchini Cyprus Costas Papacostas amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela kwa kuhusika na mripuko katika ghala moja ya risasi kwenye kituo cha jeshi la majini ambapo watu 13 waliuawa.


Papacostas mwenye umri wa miaka 74 hakuweko mahakamani wakati wa hukumu hiyo kwa kuwa tangu alipopatikana na hatia mwezi uliopita yu mgonjwa na amelazwa hospitali. Amepatikana na hatia ya  kusababisha vifo. Mripuko huo ulitokea Julai mwaka 2011 ulisababisha hasara ya  dola bilioni 4 . Ghala hiyo ya risasi iliripuka kutokana  hali ya hewa ya joto kali kisiwani humo.

No comments:

Post a Comment