- KINANA AWEKA HISTORIA KATIKA VIWANJA VYA SHIRATI OBWERE
- MAELFU YA WATU WAFURIKA KUMSIKILIZA KATIBU MKUU
- VIONGOZI 43 KUTOKA UPINZANI WARUDISHA KADI
- WANACHAMA 126 WAJIUNGA HAPO HAPO
Mbunge wa
Rorya Ndugu Lameck Okambo Airo akihutubia wakazi wa Shiratu waliofurika
kwenye uwanja wa Shiratu Obwere,Mbunge huyo alieleza jinsi gani
amefanikiwa kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa wa Geita Ndugu Joseph Musukuma akiwasalimu wakazi wa
Shiratu ,na kuwapongeza wananchi wa wilaya ya Rorya kwa umoja na
mshikamano walio nao.(P.T)
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Wanawake nchini Ndugu Amina Makilagi akihutubia wakazi
wa Shiratu kwenye mkutano wa hadhara ambao mgeni Rasmi alikuwa Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Katibu wa
NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Shiratu wilaya ya
Rorya na kuwataka wananchi hao kuwapuuza wanaotaka kuharibu mchakato wa
kupata Katiba Mpya kwani Mchakato wa Katiba hiyo imefuata taratibu zote
za kisheria.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Shiratu kwenye
viwanja vya Shiratu Obwere na kuwaambia wakazi wa Shiratu kuwa CCM
inatekeleza ahadi zake ilizoahidi kwa wakazi wa wilaya ya Rorya ,Katibu
Mkuu aliwaeleza wananchi hao mipango iliyofanyika na itakayofanyika kwa
ajili ya maendeleo ya wilaya hiyo,hasa katika suala zima la mradi wa
umeme vijijini,maji,shule na huduma za afya.
Sehemu ya
Umati wa watu walifurika kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana kwenye Uwanja wa Shiratu Obwere tarehe 24 Septemba
2013.
No comments:
Post a Comment